22.1 C
Dar es Salaam
Monday, July 22, 2024

Contact us: [email protected]

Wizara ya Maliasili yatakiwa kuweka mikakati kuongeza watalii

Anna Potinus – Dar es salaam

Rais John Magufuli ameitaka Wizara ya Maliasili na Utalii kuweka mikakati madhubuti ya kuongeza watalii nchini ambao ametaja baadhi ya malalamiko ambayo amekuwa akiyapata kupitia ripoti ya robo mwaka na kiitaka wizara hiyo kuhakikisha inafanya kazi masuala hayo.


Rais Magufuli ametoa kauli hiyo leo Jumanne Julai 9, wilayani Chato mkoani Geita katika uzinduzi wa Hifadhi ya Taifa ya Burigi – Chato yenye ukubwa wa kilometa za mraba 4,702.

“Ninatoa wito kwa Wizara ya Maliasili na Utalii kuendelea kujipanga na kuweka mikakati madhubuti ya kuongeza watalii nchini, miongozi mwa malalamiko ambayo nimekuwa nikiyapata ni pamoja na gharama za utalii kuwa juu, usafi kwenye hoteli na mengine mengi hivyo hamna budi kufuatilia mambo hayo,” amesema.


“Ninawasihi kuwa na utaratibu wa kufanya kaguzi mara kwa mara lakini pia wekeni mikakati ya kujenga uwezo wa waongoza watalii na kuhakikisha wote wanatambuliwa rasmi maana kuna wengine wanadanganya watalii, hakikisheni hifadhi zetu zinakuwa na mchanganyiko mzuri wa vivutio,” amesema.


Aidha amewataka watanzania kujega utamaduni wa kutembelea vivutio vya ndani hasa katika maeneo ya hifadhi zinazowazunguka ili kuiongezea nchi kipato na kukuza uchumi wa nchi ambapo ameitaka Wizara ya Maliasili na Utalii kuweka gharama nafuu kwa watalii wa ndani ili kuwezesha zoezi hilo.


“Ninahimiza Wizara kuendelea kuhamasisha utalii wa ndani ikiwemo kwa kuweka gharama za nafuu pia kwa watanzania ninawasihi kujenga utamaduni wa kutembelea vituo vyetu vya utalii pia tuanzisha hifadhi ndogo ndogo za kufuga wanyama pori,” amesema.


“Mimi ninafikiria kuanzisha hifadhi ndogo lakini nitafuga wale wanyama ambao ni wapole nisije nikajikuta nimekuwa kitoweo huko ndani, ninasisitiza Wizara hakikisheni mnaangalia gharama kwa wazawa zinakuwa chache,” amesema.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
589,000SubscribersSubscribe

Latest Articles