25.2 C
Dar es Salaam
Thursday, April 25, 2024

Contact us: [email protected]

Wizara ya Maji yakabidhi Dawasa jengo la Sh bilioni 40

=Tunu Nassor, Dar es Salaam

Wizara ya Maji imekabidhi jengo la Sh. bilioni 40 kwa Mamlaka ya Majisafi na Majitaka Dar es Salaam(Dawasa) ili litumike kama ofisi yao.

Akizungumza katika hafla ya kukabidhi leo Januari 3, Katibu Mkuu wa Wizara hiyo Profesa Kitila Mkumbo amesema imeamua kuwapa Dawasa jengo hilo kutokana na wizara hiyo kuhamia Dodoma na Dawasa kuwa ni Mamlaka ya maji kubwa kuliko zote nchini .

“Tumekabidhi mambo matatu kwa Dawasa ambayo ni uendeshaji wa mkataba wa ujenzi wa jengo hili, gharama zilizobaki za ujenzi ambazo ni asilimia 75 ya Sh bilioni 40 pamoja na matumizi ya jengo hilo,” amesema Profesa Mkumbo.

Amesema pamoja na kukabidhi mambo hayo  lakini hawajakabidhi umiliki wa jengo hilo ambao uko nje ya makubaliano hayo.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa Bodi ya Dawasa, Jenerali Mstaafu Davis Mwamunyange amesema Mamlaka hiyo inakabiliwa na changamoto ya ufinyu wa ofisi jambo ambalo linasababisha kushindwa kutekeleza baadhi ya majukumu yake kwa ufanisi

 “Changamoto hii imesababisha ugumu wa kufanya vikao vya dharura na utunzaji wa nyaraka ambapo wafanyakazi wanalazimika kusafirisha nyaraka kutoka gerezani kwenda makao makuu Mwananyamala,” amesema.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles