32.2 C
Dar es Salaam
Tuesday, November 12, 2024

Contact us: [email protected]

Wizara ya Kilimo, AGRI-CONNECT zawakutanisha wadau wa Parachichi nchini

Na Mwandishi Wetu, Iringa

Wizara ya Kilimo ikishirikiana na Programu ya AGRI-CONNECT inayofadhiliwa na
Umoja wa Ulaya (EU), imewakutanisha wadau wa tasnia ya Parachichi katika Kongamano la Kitaifa lilofanyika Machi 9 – 10, 2022 Mafinga, mkoani Iringa.

Mada kuu katika katika kongamano hilo ilikuwa ni ‘Kukuza Ushindani katika Tasnia ya Parachichi Tanzania”.

Washiriki wa kongamano hilo walikuwa ni wadau katika mnyororo wa thamani wa parachichi, hususan maafisa wa Serikali kutoka wizara na mamlaka husika, washirika wa maendeleo, watafiti, wawakilishi kutoka sekta binafsi, azaki za kiraia, taasisi za kifedha, wazalishaji, wasindikaji na wafanyabiashara.

Kwa mujibu wa waandaajiwa wa Kongamano hilo, Programu ya AGRI-CONNECT ilifanya uchambuzi kwenye mnyororo wa thamani wa horticulture, na ulibaini changamoto na fursa zitokanazo kwenye tasnia ya parachichi katika mikoa ya Nyanda za Juu Kusini.

Aidha, inakadiriwa kuwa zaidi ya wakulima 26,000 wanajihusisha kwenye kilimo cha parachichi, kati ya hao asilimia 38 wanapatikana katika mikoa ya Nyanda za Juu Kusini. Mikoa inayoongoza kwa uzalishaji parachichi ni pamoja na Njombe, Iringa, Mbeya, Songwe, Kilimanjaro, Kagera na Arusha.

Vilevile, utafiti huo ulibaini kuwa kilimo cha parachichi kinachipuka kwa kasi katika maeneo mengine hususan Ukanda wa Kusini na wa Kaskazini mwa nchi yetu.

Kwa miaka ya hivi karibuni, Tanzania imekuwa miongoni mwa wazalishaji wakubwa wa parachichi barani Afrika.

Uzalishaji wa parachichi ulifikia tani 40,000 mwaka 2019, na imekadiriwa uzalishaji kuongezeka kwa asilimia 20 kila mwaka.

Takriban asilimia 65 ya parachichi zilizozalishwa ziliuzwa kwenye soko la ndani; asilimia 14 zilibaki kwa wenye mashamba na asilimia 21 tu ndiyo ilisafirishwa nje ya nchi, hasa kwenye soko la Ulaya.

Hata hivyo, imeriportiwa kuna upotevu mkubwa baada ya mavuno wa hadi asilimia 20 kutokana na ukosefu wa ufanisi kwenye shughuli za mnyororo wa thamani. Usindikaji wa parachichi katika soko la ndani bado ni mdogo.

“Zao la parachichi ni miongoni mwa mazao yanayopewa kipaumbele na Serikali katika uzalishaji kutokana na faida yake kimazingira, kiafya na kiuchumi,” amesema Mkuu wa mkoa wa Iringa, Queen Sendiga, akimwakilisha Waziri wa Kilimo, Hussein Bashe.

Takwimu zinaonesha kuwa mauzo ya parachichi nje ya nchi yameongezeka kutoka tani 3,279 mwaka 2015 hadi tani 9,000 mwaka 2019 ambayo yaliingiza Taifa Dola za
Marekani milioni 8.5. Aidha, napenda kujulisha umma kuwa nchi yetu imepata fursa ya masoko mapya ya parachichi katika nchi za China na India.

Parachichi la Tanzania huwa tayari kwa kuuzwa nje ya nchi baada ya nchi zinazozalisha kwa wingi kumaliza mauzo yao na hivyo kuwapa wazalishaji nchini fursa ya pekee ya kufanya biashara bila ya kuwa na ushindani mkubwa.

Sambamba na hili, kuongezeka kwa mahitaji ya parachichi duniani kunaiweka Tanzania katika nafasi nzuri ya ushindani katika soko la nje. Kilimo cha kibiashara cha parachichi kinatoa mwanya wa kuongeza thamani kwenye sekta ndogo ya horticulture.

Licha ya kua na uwezo mkubwa wa kuzalisha parachichi, ushindani wa tasnia ya parachichi Tanzania unakwamishwa na; ukosefu wa ubora wa miche ya parachichi; mifumo ya kikodi isiyo rafiki; miundombinu duni ya kukusanya na kuhifadhi parachichi; miundombinu duni ya usafirishaji na kupelekea upotevu maradufu wa maparachichi.

Baadhi ya vipaumbele vya kuwezesha tasnia ya parachichi ni pamoja na kuboresha uratibu wa washiriki wa mnyororo wa thamani kutoka taasisi mbalimbali, maboresho ya sera na mfumo wa kisheria, uwezeshaji wa uidhinishaji bidhaa na usafirishaji nje ya nchi.

Kwa mantiki hiyo, Wizara ya Kilimo, kwa kushirikiana na programu ya AGRI-CONNECT ilianza mataarisho ya ‘Mpango Kazi wa Kitaifa wa Zao la Parachichi’ ambao utaainisha hatua mahususi, miongozo na ushiriki wa wadau mbalimbali kwa ajili ya kuendeleza maendeleo ya tasnia ya parachichi.

Kongamano hili limelenga kuanzisha jukwaa la parachichi kitaifa, kupata maoni mbalimbali toka kwa wadau yatakayosaidia kuandaa Mpango Kazi wa Kitaifa wa Zao la Parachichi na kuweka vipaumbele ili kukuza tasnia ya parachichi nchini. Kongamano hili litajadili mada ndogo tatu:Historia ya zao la parachichi na kitu gani tunajifunza kwa madhumuni

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
591,000SubscribersSubscribe

Latest Articles