24.2 C
Dar es Salaam
Wednesday, May 31, 2023

Contact us: [email protected]

Wizara ya Elimu kuendelea kuboresha mazingira ya kufundishia na kujifunzia

Ramadhan Hassan, Dodoma

Katika kuhakikisha Watanzania wanaandaliwa vyema kushiriki uchumi wa viwanda, Serikali inaendelea kutekeleza mipango mbalimbali ikiwemo kuboresha mazingira ya kufundishia na kujifunzia.

Hayo yameelezwa leo Juni 21, bungeni na Naibu Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia,William Ole Nasha alipokuwa akijibu swali la Mbunge wa Viti Maalum, Kiteto Koshuma(CCM).

Katika swali lake, Koshuma amesema kwamba ili kuelekea Tanzania ya Viwanda,Watanzania wanapaswa kuandaliwa vyema ili kushiriki kikamilifu katika viwanda vya ndani.

“Je,Serikali ina mkakati gani wa kuandaa wataalamu mbalimbali watakaotumika  katika kuendesha viwanda nchini?’ ameuliza Koshuma.

Akijibu swali hilo,Ole Nasha amesema ili kuhakikisha Watanzania wanaandaliwa vema kushiriki uchumi wa viwanda,Serikali inaendelea kutekeleza mipango mbalimbali ikiwemo kuboresha mazingira ya kufundishia na kujifunzia.

Amesema Serikali inaendelea na mpango wa ukarabati, ujenzi wa miundombinu,ununuzi wa vifaa vya kisasa vya kujifunzia na kufundishia na kuboresha mitaala  katika Vyuo na Taasisi za elimu.

“Kwa mfano ukarabati Vyuo vya Maendeleo ya Wananchi, ujenzi  na ukarabati  wa Vyuo vya Veta katika Mikoa na Wilaya pamoja na Vyuo vikuu nchini,”amesema.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
213,208FollowersFollow
567,000SubscribersSubscribe

Latest Articles