23.9 C
Dar es Salaam
Wednesday, April 24, 2024

Contact us: [email protected]

WIZARA YA ARDHI KUNUNUA VIFAA VYA KISASA

Hadija Omari, Lindi

Wizara ya Ardhi Nyumba na Maendele ya Makazi, imesema ili kurahisisha usimamizi wa wa ardhi na matumizi yake, imenunua vifaa vipya vya kisasa vya kupima ardhi nchi nzima.

Waziri wa Ardhi, William Lukuvi ameyasema hayo leo Jumatatu Julai 9, alipokuwa akizungumza na Kamati ya Ulinzi na Usalama ya Wilaya na Mkoa pamoja na Wakuu wa Idara kutoka Ofisi za Ardhi Kanda na Wilaya za Lindi.

Amesema wizara imeamua kufanya usimamizi wa karibu na ofisi zote za kanda kwa kupeleka wataalamu wa fani zote pamoja na kununua vifaa vya kisasa ambovyo vitarahisisha utendaji wao wa kazi.

“Tunataka kama watu wa wilayani wakitaka kupima ardhi, kupanga matumizi bora ya ardhi na kutatua migogoro basi wafike mkoani au kwenye ofisi za kanda wachukue vile vifaa bure wakatumie na kama hawana wataalamu tunao wataalamu wengi kwenye kanda zote wachukuliwe wakafanye kazi,” amesema Lukuvi.

Pamoja na mambo mengine, Lukuvi amesema katika utumiaji wa vifaa hivyo tayari wameandaa mafunzo rasmi kwa ajili ya kuwafundisha maofisa wapimaji wa kanda, mikoa na baadhi ya maofisa wa halmashauri ambayo yatafanyika Dodoma  ili kuwafundisha namna bora ya kutumia vifaa hivyo.

“Tunataka hadi kufikia mwaka 2020 vijiji vyote nchini viwe vimepimwa na kuwa na hati yake pamoja na kuwa na mpango wa matumizi bora ya ardhi,” amesema Lukuvi.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles