25.2 C
Dar es Salaam
Monday, November 29, 2021

Wizara ya Afya yatoa tahadhari virusi vya corona

Aveline Kitomary

Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia Wazee na Watoto, imetoa tahadhari kwa wananchi kuhusiana na virusi vya corona baada ya kutokea kwa mlipuko wa homa ya mafua makali inayosababishwa na kirusi hicho nchini China hivi karibuni.
Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa leo Ijumaa Januari 24 na Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano ya Serikali, Gerald Chami hadi sasa hakuna mgonjwa aliyepatika na ugonjwa huo nchini hivyo wananchi wanatakiwa kuchukua tahadhari kutokana na mwingiliano uliopo.
“Mlipuko wa homa ya mafua makali umeikuba nchi za China, Thailand, Korea Kusini, Japan na Marekani kuanzia mwanzoni mwa Desemba mwaka jana ambapo wizara imekuwa ikifuatilia kwa karibu mwenendo wa mlipuko wa ugonjwa huo tangu ulipoanza.
“Ugonjwa huo unaambukizwa kwa njia ya hewa kwa kuingia na majimaji yenye virusi kutoka kwa mtu mmoja kwa kukohoa au kupiga chafya au kwa kuhusisha majimaji au makamasi kutoka kwa mgonjwa aliyethibitishwa kuwa na ugonjwa huo.
“Hivyo wananchi wanatakiwa kuchukua tahadhari kwa kuzingatia kanuni za afya na usafi kwa dalili za mafua na kwa watu wenye historia ya kusafiri nchi zilizokumbwa na mlipuko kufunika mdomo wakati wa kukohoa au kupiga chafya kwa kitambaa safi kuepuka kugusana na mgonjwa mwenye dalili,” imesema taarifa hiyo.
Pamoja na mambo mengine wananchi wametakiwa pia kuzingatia usafi binafsi na kuwahi katika vituo afya endapo ataona dalili hizo na kwenda kwenye kituo cha huduma za afya zilizopo karibu na mgonjwa.
Tayari wagonjwa 560 wamethibitishwa kuathiriwa na ugonjwa huo nchini China huku wengine 17 wamefariki kutokana na ugonjwa huo.
Dalili za ugonjwa huo ni pamoja na homa na mafua makali, kuumwa kichwa, mwili kuchoka, kikohozi, kubanwa mbavu, maumivu ya misuli, vidonda vya koo, kuathiri mapafu, kupumua kwa shida na hadi kifo,” amesema Chami.

- Advertisement -
bestbettingafrica

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

66,457FansLike
167,301FollowersFollow
526,000SubscribersSubscribe
- Advertisement -
10Bet

Latest Articles