Witness: Wanaounda makundi hawajipangi

0
1327

Kibonge mwepesiNA THERESIA GASPER

WITNESS Mwaijaga ‘Kibonge Mwepesi’, amesema hali ya baadhi ya makundi ya wasanii kutodumu kwa muda mrefu inatokana na kutojipanga vizuri.

Witness alisema imekuwa kawaida kwa makundi hayo kutokudumu kutokana na kutopanga mipango yao mapema na kutoelewana.

“Makundi huwa yanaanza vizuri lakini baada ya kutoa wimbo au video wanasahau kuwa na makubaliano ya kazi zao zinavyokwenda baada ya mafanikio wanaanza migogoro kwa kuwa hawakujitambua kabla hawajaanza,” alisema.

Hata hivyo, alishauri kitu kitakachosaidia makundi kudumu na kuendelea ni maelewano na mipango mizuri kabla ya kuanza kazi zao.

 

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here