23.6 C
Dar es Salaam
Friday, March 24, 2023

Contact us: [email protected]

WinPrincess Bet yawapa Ubalozi Joti, Gigi Money

Na Jeremia Ernest, Mtanzania Digital

KAMPUNI ya Michezo ya kubashiri nchini Tanzania ya WinPrincess Bet imewapa Ubalozi Wasanii, Lucas Mhuvile maarufu ‘Joti’ na msanii wa Muziki wa Bongofleva, Gift Stanford maarufu ‘Gigy Money’.

Akizungumza katika hafla ya kuwatangaza mabalozi hao iliyofanyika Machi 7, 2023 jijini Dar es Salaam Meneja wa Mchezo wa Kubashiri wa WinPrincess nchini, Hakan Aric, amesema kampuni imekuja kivingine kwa wateja wake nakwamba kila atakayebashiri kuanzia Sh 1,000 atajionea mwenyewe kwani ina zawadi nono hiyo ni kampeni mpya ya “Ushindi Papo Hapo” (“Immediate Pay-Out”) katika kuweka dau mtandaoni.

“WinPrincess Online Platform inakaribisha watu wote wazoefu na wapya kubashiri kwa njia ya mtandaoni kupitia kampuni hii yenye jumla ya uzoefu wa miaka saba katika kwa kuweka Dau kwenye simu popote mtu alipo mtandaoni.

“Kubashiri michezo ya mpira na kasino kupitia tovuti ya WinPrincess inakuja na faida nyingi ambazo huleta msisimko wa kweli ikiwemo kuanzia kubashiri kwa kima cha chini hadi Sh 1 moja ambayo ni nafuu kwa kila Mtanzania kuanzia miaka 18 na kuendelea, kampuni hii ina odds kubwa kuliko zile zilizopo hapa nchini,” amesema Aric.

Ameongeza “Ikiwa na lengo la kujali maslahi ya wateja, kuwapa ofa ya asilimia 100 kwa kila mchezaji mpya, uwezo wa kubet mchezo mmoja hadi 40, kutoa bonasi kupitia bahati nasibu zetu na bonasi za kurejesha pesa yote pamoja na mpango wa uaminifu unaoturuhusu kuwatuza wateja wetu wa kwa waaminifu bila longolongo,’ amesmea.

Aric pia amemshukuru Mkurugenzi Mkuu wa Bodi ya Michezo ya Kubahatisha Tanzania(GBT), James Mbalwe kwa kutuma mwakilishi kuwa nao katika siku hiyo muhimu, ambapo pia ameishukuru Africa Princess Casino ambayo ni kampuni dada yao kwa kuwa mwekezaji wao.

Naye Mwakilishi kutoka Bodi ya Michezo ya Kubahatisha Tanzania, Regaliva Martine amewashauri watu wote wanaobashiri kuwa na kiasi na kuwa makini kwani kuna muda wa kufanya kazi za kujiingizia kipato, hivyo watumie muda wao vizuri

Kwa upande wake Meneja Masoko wa Tele-Marketing kutoka WinPrincess Sports Betting, Winny Macha amesema amesema wanamatarajio makubwa sana jamii itawapokea kwani wamekuwa kila mwisho wa mwaka wanadisha shukrani kwa jamii kwa kutembelea vituo mbalimbali vya watoto yatima kwa kutoa misaada hivyo .

“Sisi kama WinPrincess tunaamini katika uaminifu na tuko hapa kutoa imani kwa wateja wetu kwa kutangaza kauli mbiu yetu “Ushindi ni Papo Hapo” ambayo ina maana mshindi ana uhakika wa Malipo Papo Hapo kutokana na ushindi wake.

“Tuanapoadhimisha siku ya kimataifa ya wanawake, tunapenda kuwakaribisha wanachama wapya, hasa wanawake kuja kujaribu jukwaa letu na kujiburudisha kwa hali ya kawaida ya kushinda na kupata zaidi. Odds Bora na malipo papo hapo,” amesema.

Naye Msanii Gigy Money ameshukuru kwa kupewa ubalozi huo ambapo ameahidi kuitangaza na kuhakikisha wateja wapya wanapatikana hivyo wanawake vijana na makundi yote waitumie kampuni hiyo kubashiri ina zawadi nono

Aidha, Meneja wa Msaanii Joti, Peter Mkoba ameshukuru kampuni hiyo kwa kumuamini Joti na kumfanya kuwa balozi ambapo ameeleza kuwa msanii huyo ataitangaza kwa nguvu zake zote.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
211,070FollowersFollow
563,000SubscribersSubscribe

Latest Articles