29.2 C
Dar es Salaam
Wednesday, October 20, 2021

WINGU ZITO RIPOTI YA FARU JOHN

Na Masyaga Matinyi


IMETHIBITIKA kuwa Mkurugenzi wa Wanyamapori aliridhia kuhamishwa Faru John, kinyume cha ripoti iliyowasilishwa kwa Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa, Jumatatu iliyopita.

Ripoti hiyo iliyokabidhiwa kwa Waziri Mkuu na Mwenyekiti wa Tume iliyoundwa na Serikali kuchunguza taarifa za kifo cha Faru John, ambaye ni Mkemia Mkuu, Profesa Samweli Manyele, ilidai faru huyo alihamishwa bila kibali cha Mkurugenzi wa Wanyamapori.

Faru John alihamishwa kutoka Hifadhi ya Ngorongoro Desemba 8, 2015 na kupelekwa eneo la Sasakwa Grumeti, Wilaya ya Serengeti, baada ya mchakato uliochukua takribani miaka 13.

Profesa Manyele alisema tume yake ilifanya uchunguzi wa kifo cha mnyama huyo kwa kupima vinasaba vya sampuli mbalimbali vikiwemo mzoga, fuvu, mifupa, pembe, damu, ngozi na kinyesi kilichokaushwa, ambapo ilibainika kuwa vyote ni vya mnyama mmoja, aina ya faru mweusi ambaye ni dume.

Alisema matokeo hayo yamethibitisha kuwa Faru John alikufa katika hifadhi ya Sasa kwa Grumeti.

Akibainisha mapungufu katika kumhamisha mnyama huyo, alisema ni kutokuwepo kwa kibali rasmi cha kumhamisha, kukosekana kwa mkataba wa kupokelewa kwa Faru John hifadhi ya Sasakwa Grumeti.

Mtanzania limefanikiwa kupata nakala ya barua iliyoandikwa Septemba 25, 2015 kutoka kwa aliyekuwa Kaimu Mkurugenzi wa Wanyamapori, H.W. Keraryo, kwenda kwa Mratibu wa Taifa wa Faru na Tembo, barua ambayo iliridhia kuhamishwa kwa faru huyo.

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

66,457FansLike
162,594FollowersFollow
522,000SubscribersSubscribe

Latest Articles