24.2 C
Dar es Salaam
Friday, April 19, 2024

Contact us: [email protected]

WIMBO WA NEY WA MITEGO

Verse 1:

Unachokipanda leo ndicho utachovuna kesho. 

Imeandikwa Mwanaume kula kwa jasho. 

Najiuliza hivi ni nani kaiona kesho. 

Chapa mwendo na ukilala hauna chako. 

Hivi uhuru wa kuongea kwenye hii nchi bado upo?.

Usije kuongea vitu kesho ukajikuta sentro. 

 

Chorus:

Kuna viongozi wavuta bangi? "wapo "

Maana wana maamuzi ya kise…. "wapo"

Kuna walio mmiss Jakaya? "wapo"

Walio choka kuisoma namba? "wapo"

Kuna walio poteza malinda? "wapo"

Kuna wasanii mateja? "wapo"

Kuna mademu wanasagana? "wapo"

Kuna vidume wanalelewa? "wapo"

Kuna wasanii wanalogana? "wapo"

 

Verse 2

Kuna Radio na Tv, naona zimeshapoteza CV.

Hakuna uhuru wa habari, wala taarifa ya habari. 

Wanapindisha pindisha tu kuiogopa serikali. 

Siamini nchi inaendeshwa na kiki. 

Siasa inafunika mziki. 

Viongozi wanashindana kukiki. 

Wanagombea front page, wauze kwenye gazeti. 

Nasikia kuna viongozi wamefoji vyeti. 

 

Verse 3 

Kiongozi mwenye busara anapokea ushauri. 

Anapokea mawazo,haweki mbele kiburi. 

Hey! Samahani mheshimiwa, hivi unamjua BASHITE?. 

hili ni jipu jipya toka kolomije. 

Limesha iva na usaa, limeshatunga. 

Na kukabidhi sindano ya kulidunga. 

Daktari haogopi ukubwa wa kidonda. 

We_si Dr wa majipu, tumbua hakuna kuvunga. 

Kuvamia ofisi za watu kumbe nayo ni kazi. 

Hakuna noma wanangu pigeni kazi. 

Boda boda kazi,  bajaji Kazi.

Eti!  Vipi? Kukaba nayo kazi?. 

Refa ni wao piga manati. 

Vita ya Masai na mmang'ati. 

Biashara ya ngono na Super shafti. 

Pumzi imekata nashika shati…

 

Hahahahahaha! Wewe mtu gani sasa…… 

Hutaki kushauriwa, hutaki kukosolewa…… 

Umelogwa wewe,…….. 

unajiona ndugu yake na  Yesu ee….

Oya! Wanangu eeeh! Round hii mtanyooka haki ya Mungu. 

Naona kichaa kapewa Rungu..

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles