ZIPO taarifa zinazodai Arsenal wanaweza kukaa mezani na Jack Wilshere ili kujadili uwezekano wa kiungo huyo kuvaa tena ‘uzi’ wa Washika Bunduki hao wa jijini London.
Wilshere mwenye umri wa miaka 29, hana timu tangu alipoachwa na Bournemouth mwishoni mwa msimu uliopita.
Taarifa zinadai kuwa kocha wa Arsenal, Mikel Arteta, amefungua mlango kwa mchezaji mwenzake huyo wa zamani kurejea Emirates.
Akimzungumzia Arteta aliyewahi kucheza naye Arsenal, Wilshere amesema: “Nilifurahia kucheza naye na kuwa pamoja kwenye chumba cha kubadilishia nguo. Kusikia anasema mlango uko wazi (kwangu kurudi) ni jambo zuri.