WILL SMITH ANYOA RASTA ZA MTOTO WAKE

0
764

NEW YORK, MAREKANI


NYOTA wa filamu na muziki nchini Marekani, Will Smith, amemnyoa mtoto wake rasta Jaden Smith, huku akimtaka aachane na mtindo huo wa nywele kwa kuwa unampendeza dada yake, Willow Smith na si yeye.

Jaden mwenye miaka 18, alikuwa na rasta kama dada yake, Willow mwenye umri wa miaka 17, hivyo baba yao Smith alimtaka Jaden kuzinyoa nywele hizo na kumwacha dada yake peke yake.

“Nimekubali kumwacha dada yangu aendelee na nywele zake za rasta za kwangu nilizipenda sana lakini nadhani baba hakutaka niwe hivyo na ndio maana kila siku alikuwa ananiambia nizitoe.

“Kwa sasa baba ana furaha sana baada ya kuona nimezitoa na sasa ninarudi kwenye mwonekano wangu wa zamani,” alieleza Jaden.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here