22 C
Dar es Salaam
Sunday, June 4, 2023

Contact us: [email protected]

WIKI YA ELIMU KWA MLIPAKODI KUFANYIKA MACHI

Na Veronica Kazimoto, Dar es Salaam

Wiki ya Elimu kwa Mlipakodi ambayo Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), huitumia kuelimisha, kusikiliza malalamiko, changamoto pamoja na kupokea mrejesho na maoni mbalimbali kutoka kwa walipakodi itafanyika Machi 5 hadi 9 mwaka huu, katika mikoa yote nchini.

Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo Jumanne Februari 27, Mkurugenzi wa Huduma na Elimu kwa Mlipakodi, Richard Kayombo amesema wiki hii ya Elimu kwa Mlipakodi kwa sasa itakuwa inafanyika kila baada ya miezi mitatu ambapo pamoja na mambo mengine wananchi watapata fursa ya kuongeza uelewa juu ya masuala mbalimbali yanayohusu kodi.

“Katika wiki hiyo, mamlaka itafundisha mada mbalimbali kama vile ulipaji wa Kodi ya Majengo kwa njia ya kieletroniki ikiwa ni pamoja na kuwakumbusha wamiliki wa majengo kulipa kodi hiyo kabla ya Juni 30, mwaka huu ili kuepuka usumbufu.

“Kwa wafanyabiashara watafundishwa kwa undani juu ya Mkataba wa Huduma kwa Mlipakodi ambao umeainisha haki na wajibu wa mlipakodi na viwango vya huduma wanavyopaswa kupata kutoka TRA.

“Mada nyingine itakayofundishwa katika wiki hiyo ni pamoja na matumizi sahihi na umuhimu wa kutumia Mashine za Kielektroniki za Kutolea Risiti (EFDs) ambapo wananchi watakumbushwa na kusisitizwa suala zima la kutoa na kudai risiti kila wanapouza au kununua bidhaa na huduma mbalimbali,” amsema Kayombo.

Pamoja na mambo mengine, shughuli nyingine zitakazofanyika katika wiki hiyo ni pamoja na usajili wa walipakodi wapya ikiwa ni moja ya dhamira ya TRA kuhakikisha inasajili walipakodi wapya 1,000,000 nchi nzima katika mwaka huu wa fedha wa 2017/18.

“Natoa wito kwa wananchi wote kutumia fursa hii ili waweze kujifunza kwa kina mambo mbalimbali yanayohusu kodi na ukusanyaji wa mapato ya Serikali kwa ujumla,” amesema Kayombo.

 

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
213,284FollowersFollow
568,000SubscribersSubscribe

Latest Articles