30 C
Dar es Salaam
Monday, September 27, 2021

WHO yashauri uvaaji barakoa sehemu za mikusanyiko

GENEVA, USWISI

SHIRIKA la Afya Duniani (WHO) limebadili ushauri wake kuhusu uvaaji wa barakoa, likisema ni lazima zivaliwe kwenye mikusanyiko ya watu ili kusaidia kutosambaa kwa virusi vya corona.

WHO imesema taarifa mpya zinaonyesha barakoa inaweza kutoa kizuizi cha matone yanayoweza kuambukiza.

Baadhi ya nchi duniani tayari zilikwishawaambia wananchi wake wavae barakoa sehemu zenye mikusanyiko.

Awali WHO ilisema hakukuwa na ushahidi unaojitosheleza kwamba watu ambao hawana virusi hivyo wavae barakoa.

Dk. Maria Van Kerkhove, ambaye anaongoza dawati la ufundi kuhusu Covid-19, aliliambia shirika la habari la Reuters kwamba pendekezo lilikuwa ni  watu ‘kuvaa barakoa za kitambaa (za kushona), na si zile zinazotumika mahospitalini’ katika maeneo  ambayo yana hatari kubwa ya kuenea kwa virusi vya corona. 

Shirika hilo lilikuwa likishauri  kwamba watu wanaopaswa kuvaa barakoa zile za hospitali   ni wale wagonjwa au wale wanaowahudumia.

Duniani kote kuna watu waliothibitika kuugua virusi vya corona wamefika milioni 6.7 na karibu vifo 400,000 tangu ugonjwa huo uzuke mwaka jana, kwa mujibu wa takwimu zilizokusanywa na Chuo Kikuu cha Johns Hopkins.

WHO imesema maelekezo hayo mapya kuhusu uvaaji wa barakoa yamechagizwa na tafiti za wiki za hivi karibuni. 

“Tunashauri serikali kuhamisha umma kuvaa barakoa,” Dk. Van Kerkhove alisema.

Baadhi ya wachambuzi wameilezea hatua hiyo ya WHO kama mabadiliko makubwa katika maelekezo yake ukilinganisha na yale ya awali.

Kwa miezi kadhaa sasa, wataalam wa shirika hilo walishikiria msimamo kwamba barakoa zinaweza kuhamasisha hisia ya uwongo ya usalama na ingewanyima wataalamu wa matibabu vifaa vya kinga vinavyohitajika sana.

Wakati hoja kama hizo zikiwa hazijapita wakati huo huo WHO imekuja na jambo jipya kwamba ushahidi mpya umebainika ju ya hatari ya maambukizi.

Kwamba utafiti mpya unaonyesha mtu anaweza kupata maambukizi makubwa siku chache kabla ya kuonyesha dalili na kwamba wapo wanaoweza kupata virusi hivyo na kutoonyesha kabisa dalili.

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

66,457FansLike
158,348FollowersFollow
519,000SubscribersSubscribe

Latest Articles