29.2 C
Dar es Salaam
Tuesday, September 28, 2021

WHO yahofia corona kuenea kimya kimya

BRUSSELS, UBELGIJI

SHIRIKA la Afya Duniani (WHO) linasema ingawa Afrika ndilo eneo ambalo lina idadi ndogo zaidi ya waathirika wa ugonjwa wa Covid-19 lakini kuna wasi wasi kuwa ugonjwa huo utaenea kimya kimya iwapo viongozi wa bara hilo hawatalipa umuhimu suala ya vipimo.

Mjumbe wa WHO, Samba Sow alitahadahrisha kuwa ukosefu wa vipimo huenda ukapelekea janga la Covid-19 kuenea kimya kimya barani Afrika na hivyo viongozi wa bara hilo wanapaswa kulipa kipaumbele suala la vipimo.

Kwa mujibu wa takwimu za Kituo cha Kudhibiti na Kuzuia Magonjwa Afrika (Africa-CDC), hadi kufikia Mei 26 idadi ya waliofariki kutokana na Covid-19 barani Afrika walikuwa ni 3,471.

Miongoni mwa watu mashuhuri waliofariki ni Rais wa zamani wa Jamhuri ya Congo, Jacques Joachim Yhombi-Opango na Waziri Mkuu wa zamani wa Somalia, Nur Hassan Hussein. 

Aidha kwa mujibu wa takwimu hizo idadi ya walioambukizwa Covid-19 barani Afrika ni 115,346 huku 46,426 wakipona baada ya kupata matibabu.

Wataalamu wanaonya kuwa, iwapo ugonjwa huo utaenea sana Afrika basi bara hilo litashindwa kukabiliana na hali hiyo kutokana na mifumo dhaifu ya afya.

AFP

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

66,457FansLike
158,609FollowersFollow
519,000SubscribersSubscribe

Latest Articles