WHO watangaza hali ya hatari DRC

0
1110

KINSHASA, DRC

Shirika la afya la kimataifa WHO, limetangaza kuwa hatari ya maambukizi ya ugonjwa wa Ebola kuzidi kusambaa na kiwango chake kiko juu zaidi miongoni mwa wananchi wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo.

WHO limeeleza kuwa vyanzo vya maambuziko ya ugonjwa wa Ebola vimeongezeka na sasa njia za usafiri na shughuli za umma ni hatari kwa wananchi kuambukizana huku tathimini ya kusambaa kimataifa imebaki hatari ndogo.

Taarifa ya WHO imesema kuwa kitaifa na majimboni nchini humo hatari ya kuambukizana iko juu na kushauri majimbo jirani na mataifa kuimarisha tahadhari dhidi ya maradhi hayo.

Aidha WHO wamesisitiza kuendelea kushirikiana na mataifa jirani na washirika kuhakikisha mamlaka za afya zinachukua tahadhari na zinakuwa tayari kuchukua hatua.Jumanne iliyopita Naibu mkurugenzi wa WHO Peter Salama alionya taifa jirani la Uganda kuchukua tahadhari kufuatia tishio la maambukizi mpakani jirani na ziwa Albert.Kwa mujibu wa takwimu wa shirika la WHO mlipuko wa Ebola umesababisha vifo vya watu 101 tangu ulipolipuka mnamo mwezi Agosti mwaka huu.

Huu unakuwa mlipuko wa mara ya kumi kutokea nchini DRC tangu mwaka 1976, ambapo hali ya hatari iko juu sana katika jimbo la kaskazini mashariki ambako kunavikundi kadha avinavyomiliki silaha jirani na mpaka wa Uganda Rwanda na Sudani kusini.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here