27.2 C
Dar es Salaam
Tuesday, April 23, 2024

Contact us: [email protected]

WHO: Majaribio ya chanjo ya corona yameanza

BRUSSELS, UBELGIJI

SHIRIKA la Afya Duniani (WHO) limesema siku 60 baada ya sampuli za virusi vya corona au Covid -19 kuwasilishwa na China, chanjo ya kwanza ya majaribio imeanza.

Akizungumza katika mkutano na waandishi wa habari mjini Geneva, Uswisi, Mkurugenzi Mkuu wa WHO, Dk. Tedros Ghebreyesus alisema, “haya ni mafanikio makubwa, tunawapongeza watafiti kote duniani ambao wamekuja pamoja ili kutathmini majaribio ya tiba.”

Aliongeza kuwa WHO na washirika wake wanaandaa utafiti katika nchi nyingi ambako baadhi ya nchi hizo dawa hizi ambazo hazijajaribiwa zitalinganishwa.

Alisema utafiti huo mkubwa unaandaliwa ili kukusanya takwimu zinazohitajika kuonyesha matibabu yapi yanafaya kazi zaidi.

Dk. Tedros alisema mchakato huo umepewa jina la “Majaribio ya Mshikamano”.

Mkurugenzi huyo mkuu wa WHO alisema tayari nchi kadhaa zimethibitisha kwamba zitashiriki utafiti huo wa  “Mshikamano wa Majaribio” zikiwemo Argentina, Bahrain, Canada, Ufaransa, Iran, Norway, Afrika Kusini, Hispania, Uswisi na Thailand na amesema anaamini nchi nyingine nyingi zitajiunga.

Dk. Tedros aliongeza kuwa mfuko wa hatua za mshikamano dhidi ya Covid -19 hadi sasa umeshakusanya zaidi ya Dola milioni 43 kutoka kwa watu zaidi ya 173,000 na mashirika ikiwa ni siku chache tu tangu ulipozinduliwa.

Alisisitiza kwamba virusi hivi ni tishio kubwa lakini pia ni fursa ya kuja pamoja kukabiliana na adui huyu mkubwa dhidi ya ubinadamu.

Mkurugenzi

Katika taarifa, kamati ya msikiti huo ilisema: “Baada ya mashauriano na Baraza la Maulamaa wa Msikiti wa Jamia na pia kufuatia mashauriano na Jumuiya ya Waislamu Wanaofanya Kazi za Kitaalamu katika Sekta ya Tiba (KAMMP), Kamati ya Msikiti wa Jamia imeamua kuwa, kuanzia Jumatano Machi 18, sala zote za jamaa zitasitishwa kwa muda katika Msikiti wa Jamia.”

Aidha Msitiki wa Al Huda katika mtaa wa South B Nairobi nao pia umetoa taarifa na kusema kufuatia agizo la Serikali la kupiga marufuku mijumuiko ili kuzuia kuenea ugonjwa wa Covid 19, kamati ya msikiti imeamua kuwa sala zote zitasitishwa kwa muda kuanzia Machi 19.

Hali kadhalika kamati ya Msikiti wa Parklands mjini Nairobi imesema msikiti huo utafungwa kwa muda ili kuzuia maambukizi ya kirusi cha corona. Vile vile msikiti wa mtaa wa Hurlingham, Masjid ur Rahma nao pia umetangaza kufunga milango yake kwa muda.

Nayo kamati ya Masjid Imtiaz imetangaza kuwa msikiti huo ambao pia uko kati kati ya jiji la Nairobi nao pia umefungwa kwa muda. Katika taarifa, mwenyekiti wa kamati ya msikiti huo Rafiq Miyanji alisema baada ya mashauriano na wanazuoni na wataalamu wa tiba, wameamua kufunga msikiti ili kuzuia kuenea ugonjwa wa corona.

Hadi sasa watu saba wameambukizwa ugonjwa wa Covid 19 nchini Kenya na hivyo kuna hofu kuwa homa hiyo hatari itaenea kwa kasi iwapo hatua za haraka hazitachukuliwa.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles