24.2 C
Dar es Salaam
Monday, September 26, 2022

WHO: KUUMWA NA NYOKA KUPEWE KIPAUMBELE

GENEVA, USWISI


NCHI wanachama wa mkutano wa Shirika la Afya Duniani (WHO) wamepitisha azimio la kutambua kuumwa na nyoka kuwa ni suala linalohitaji kupewa kipaumbele katika kulishughulikia.

Maelfu ya watu hufa kila mwaka na wengine kupata ulemavu kutokana sumu inayotokana na shambulio la nyoka.

WHO inasema athari zinazotokana na kuumwa na nyoka zimeendelea kuwa moja kati ya magonjwa ya kitropiki ambayo hayatiliwi maanani.

Kufikiwa makubaliano hayo kwa nchi wanachama wa WHO, kuna nia ya kuhakikisha kunakuwepo mbinu za kuzuia, kutibu na kukabili mashambulizi ya nyoka.

Makundi ya mbalimbali ya wanaharakati wa masuala ya afya yamesifia azimio hilo na kusema hatua hiyo inafungua milango katika kupunguza vifo na ulemavu duniani kote.

WHO kwa sasa lina jukumu la kuja na mpango wa pamoja kuimarisha programu za tiba, kuzuia na kurekebisha.

Hii itahusisha kutoa dawa za kupambana na sumu kwa bei rahisi, dawa ambazo ilikua gharama kupatikana kwenye nchi zilizo masikini hasa kusini mwa jangwa la Sahara.

Hali ya umaskini na kutokuwa na vituo vya afya vinavyokidhi mahitaji kumesababisha vifo vya maelfu ya watu huku wengine wakitafuta tiba ya kienyeji ambayo husababisha madhara zaidi.

Lakini mpango huu mpya utalenga kuwafundisha watoa huduma wa afya jinsi ya kushughulikia mtu aliyeumwa na nyoka na elimu ya huduma ya kwanza kwa jamii iliyo hatarini.

Kila mwaka zaidi ya watu 100,000 hufa duniani kutokana na kuumwa na nyoka asilimia 20 wakitoka barani Afrika.

Karibu watu nusu milioni wana ulemavu wa kutokuona, kukatwa viungo na ulemavu mwingine kutokana na mashambulizi ya nyoka.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
202,051FollowersFollow
554,000SubscribersSubscribe

Latest Articles