24.2 C
Dar es Salaam
Sunday, September 25, 2022

WHO KUFANYA MAJARIBIO YA CHANJO YA EBOLA

SHIRIKA la Afya Duniani (WHO), wiki hii linakusudia kuanza kufanya majaribio ya chanjo dhidi ya ugonjwa wa ebola ambao umezuka tena huko Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC).

Mwishoni mwa wiki jana, Mkurugenzi wa WHO,  Tedros Adhanom alitembelea katika mji wa Bikoro kaskazini magharibi mwa nchi hiyo, kujionea hali halisi na kufanya tathmini namna ya kudhibiti maambukizi ya ugonjwa huo.

Kwa mujibu wa Shirika la Utangazaji BBC, tangu kuripotiwa kwa ugonjwa huo nchini humo tangu Aprili 4, mwaka huu kumeripotiwa zaidi ya visa 30 ambavyo huenda ni vya ugonjwa wa Ebola.

Watu wapatao 18 wamefariki dunia licha ya kwamba ni visa viwili tu vilivyothibitishwa kutokana na Ebola.

WHO hivi sasa inafuatilia kwa ukaribu mlipuko huo wa ugonjwa ambao unaambukizwa kwa njia ya kugusa majimaji yaliyotoka kwa mgonjwa.

Pamoja na mambo mengine, hofu iliyopo sasa ni wapi pengine ugonjwa huo utazuka na kuathiri maeneo mengine duniani, hivyo WHO tayari mashirika mengine yanayofanya kazi nchini humo na yale ya Umoja wa Mataifa yameanza kutuma timu ya waangalizi wao nchini humo ili kufuatilia na kudhibiti usienee katika maeneo mengine.

Inaelezwa kuwa njia mojawapo ya kuudhibiti ugonjwa huo ni kufuatilia kwa ukaribu na kuwatenga wale wanaogundulika kuwa na maambukizi hayo na kuwaweka katika mpango wa ufuatiliaji, na yeyote anayekuwa kwenye hatari ya kuambukizwa anafuatiliwa kwa siku 21 na maziko hufanyika kwa uangalizi ili kuudhibiti.

Virusi vya Ebola viligunduliwa katika miaka ya nyuma mnamo 1976 katika milipuko miwili ambapo watu 151 walifariki katika enoe la Nzara, Sudan kusini na watu 280 waliofariki katika eneo la Yambuku karibu na mto Ebola uliopewa jina kutokana na ugonjwa huo.

Dunia haiwezi kusahau janga la Afrika magharibi mnamo 2014-16 lililozuka katika kijiji kimoja cha mpakani nchini Guinea, na muathiriwa wa kwanza anadhaniwa kuwa mtoto wa kiume mwenye umri wa miaka miwili aliyefariki duniani mwaka 2013.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
201,853FollowersFollow
553,000SubscribersSubscribe

Latest Articles