WHO: Kifua kikuu ndio ugonjwa hatari zaidi duniani

0
714

BRUSSELS, UBELGIJI

WAKATI idadi ya vifo kutokana na virusi vya corona ikiendelea kupanda, maafisa wa afya ulimwenguni wanakumbusha kuwa ugonjwa wa kifua kikuu ndio ugonjwa hatari kabisa wa kuambukiza kote duniani. 

Kwa mujibu wa ripoti iliyotolewa jana na Umoja wa Mataifa (UN), ugonjwa wa kifua kikuu huwaua watu zaidi kuliko ugonjwa mwingine wowote wa kuambukiza. 

Jana, ikiwa ni siku ya Kimataifa ya kupambana na ugonjwa wa Kifua Kikuu, Shirika la Afya Ulimwenguni (WHO) lilisema kuwa karibu watu milioni 1.5 waliaga dunia kutokana na ugonjwa huo mwaka wa 2018. 

WHO ilisema karibu watu milioni 10 huambukizwa kifua kikuu kila mwaka ikiongeza kuwa zaidi ya watu 4,000 hufariki dunia kila siku kutokana na ugonjwa wa kifua kikuu. 

Mkurugenzi Mkuu wa WHO, Tedros Ghebreyesous alisema kuwa janga la sasa la virusi vya corona linadhihirisha namna wagonjwa wenye matatizo ya mapafu au mifumo dhaifu ya kinga mwilini walivyo katika hatari kubwa kutokana na mripuko huo mpya.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here