22.7 C
Dar es Salaam
Sunday, June 4, 2023

Contact us: [email protected]

WHO: ELIMISHENI JAMII KUEPUKA MAGONJWA YA MLIPUKO

Veronica Romwald, Aliyekuwa Nairobi

Waandishi wa habari wa masuala ya afya Barani Afrika, wamehimizwa kujikita zaidi kuelimisha jamii namna ya kuepukana na magonjwa ya mlipuko badala ya kusubiri yatokee ndipo watoe habari.

Rai hiyo imetolewa Nairobi na Ofisa Mfuatiliaji wa Masuala ya Majanga (IHE – Kenya) wa Shirika la Afya Duniani (WHO), Dk. Freddy Banza alipowasilisha mada katika semina ya waandishi wa habari za afya iliyolenga kuwajengea uwezo wa namna bora ya kuripoti masuala ya majanga ya dharura.

“Kweli mnafanya kazi nzuri, mnajitahidi kuelimisha jamii  kuhusu magonjwa mbalimbali, ila kuna changamoto tumeona, jamii nyingi zinahitaji elimu namna ya kuepukana na majanga na magonjwa ya mlipuko.

“Ni vema mkijikita hapo, badala ya kusubiri yatokee ndipo mjikite kutoa habari, tuweke msingi mzuri utakaosaidia jamii zetu,” amesema.

Pamoja na mambo mengine, Dk. Banza amewataka waandishi hao kufanya tafiti za kina na mahojiano kwa watu wanaostahili, ambao watawapatia taarifa sahihi ili kusaidia jamii zao.

Amesema WHO imeweka Idara maalumu ya ufuatiliaji wa magonjwa na majanga ya dharura katika kila nchi ambazo zinashirikiana kwa ukaribu na Wizara za Afya katika ufuatiliaji huo.

Semina hiyo iliyoandiwa na WHO kanda ya Afrika, ilijumuisha waandishi wa habari waliojikita kuandika masuala ya afya wa Tanzania, Kenya, Uganda, Ghana, Ethiopia, Mozambique, Zambia na Cameroon

 

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
213,283FollowersFollow
568,000SubscribersSubscribe

Latest Articles