25.4 C
Dar es Salaam
Saturday, November 16, 2024

Contact us: [email protected]

WHI yajivunia mafanikio ‘Faida Fund’

Na Hassan Daudi, Mtanzania Digital

MAUZO ya vipande katika Mfuko wa Faida (Faida Fund) unaoendeshwa na Watumishi Housing Investment (WHI) yamevuna Sh bilioni 12.95, ukilinganisha na Sh bilioni 7.5 zilizotarajiwa kukusanywa.

Afisa Masoko na Mawasiliano Shirika la Watumishi Housing Investiment(WHI), Maryjane Makawia akitoa maelezo kwa waandishi wa habari kabla ya kuanza kwa mkutano huo Januari 12, 2023 jijini Dar es Salaam.

Faida Fund ni mfuko wa uwekezaji wa pamoja unaoendeshwa na taasisi hiyo ya Serikali ya uendeshaji Milki (Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora) inayosimamia uwekezaji.

Aidha, huku Benki ya CRDB ikiwa Mtunza Dhamana wa Mfuko wa Faida, mafanikio hayo yamepatikana ndani ya mwaka mmoja tu, tangu mauzo ya vipande yalipofunguliwa Novemba Mosi, mwaka jana.

Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo Januari 12, 2023, Afisa Mtendaji Mkuu wa Watumishi Housing, Dk. Fred Msemwa, anasema lengo la kuanzishwa kwa Mfuko wa Faida ni kutoa fursa kwa wawekezaji wa Tanzania.

“Kwa awali, tulitarajia kupata bilioni 7. 5 lakini hadi tunafunga, Desemba 31, mwaka jana, tulishakusanya bilioni 12.95. Ni sawa na mafanikio ya asilimia 173,” anasema Dk. Msemwa.

Katika hatua nyingine, Dk. Msemwa amefichua kuwa bado Mfuko wa Faida umeendelea kuwatia wawekezaji wengi, akitaja idadi ya waliojiandikisha hadi sasa kuwa ni 3,800.

“Katika hao, 800 tayari wameshawekeza, huku waliobaki wakiwa wameshajisajili. Idadi hiyo inajumuhisha wawekezaji wa aina tatu tunaopokea.

Hapo kuna mmoja mmoja, vikundi, watoto (kwa kusimamiwa na wazazi) na taasisi. Hii inatoa picha kwamba Mfuko unakua kwa kasi na hadi sasa idadi haiko hivyo, imeshapanda sana.

Wakati huo huo, Dk. Msemwa aliweka bayana siri za hatua kubwa hiyo waliyopiga ndani ya muda mfupi. Ni zipi hizo?

“Kwanza, niseme mafanikio haya yametokana na imani kubwa waliyonayo wawekezaji kwetu sisi. Kama si kutuamini, ingekuwa ngumu kufika hapa tulipo,” amesema.

Mbali ya hilo, pia Dk. Msemwa aliitaja teknolojia kuwa na mchango mkubwa katika mafanikio yao. Katika hilo, alipigia mfano mtandao wa malipo serikalini, akisema imekuwa rahisi kwa wawekezaji kujisajili kupitia simu au kompyuta.

“Hii imeondoa usumbufu kwa kuwa sasa mtu anaweza kufanya kila kitu akiwa na simu yake ya mkononi. Kuanzia kujisajili, hadi kufanya huduma zingine. Imerahisisha sana wawekezaji kutufikia,” amesema.

“Tatu, ni ninyi waandishi wa habari. Niseme tu, mmefanya kazi kubwa mno kuelimisha watu juu ya faida za kuwekeza. Si tu kuwekeza, pia mmetufanya tufahamike kwa hao wawekezaji. Leo hii, tumefika hapa kwa sababu na ninyi mlifanya kazi kubwa.

Kwa upande mwingine, Dk. Msemwa amesema WHI haifikirii kubweteka kwa mafanikio hayo na badala yake wamejipanga kuhakikisha wanavuna wawekezaji wengi zaidi.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
591,000SubscribersSubscribe

Latest Articles