27.7 C
Dar es Salaam
Monday, December 16, 2024

Contact us: [email protected]

WHI yaanza kutekeleza agizo la Waziri mradi Magomeni

Na Faraja Masinde, Mtanzania Digital

Taasisi ya Nyumba ya Watumishi Housing Investments (WHI) imenza kutekeleza agizo la Serikali la kubadilisha matumizi ya flemu za biashara kuwa nyumba katika mradi wa Magomeni jijini Dar es Salaam.

Itakumbukwa agizo hilo lililotolewa Jumanne Septemba 27, 2022 na Waziri wa Ofisi ya Rais- Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Jenista Mhagama alipotembelea mradi huo uliopo Magomeni Usalama jijini Dar es Salaam.

Waziri Mhagama alisema nini?

Akiwa katika ziara hiyo Waziri Mhagama alitoa kipindi cha miezi sita kwa WHI kubadilisha matumizi ya sakafu ya kwanza (First Floor) kutoka kuwa eneo la biashara hadi makazi.

“Natoa miezi sita kwa Watumishi Housing kuhakikisha mnabadili matumizi ya hizi flemu nane za biashara ambazo hadi sasa hazijapata wapangaji kuhakikisha zinakuwa nyumba za kawaida.

“Hivyo, kwa hesabu hiyo ya nyumba nane ukijumlisha na hizi 88 itakuwa 96, ni matumaini yangu kuwa hili mtalitekeleza ndani ya muda huu tuliopeana,” alisema Mhagama.

Awali, akizungumza wakati wa ziara hiyo Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa WHI, Paskali Massawe akizungumzia mradi huo wa Magomeni alisema nyumba zote 88 zimenunuliwa na watumishi wa umma huku akiahidi kufanya ukarabati wa nyumba nane za floor ya kwanza zitakazo fanya jumla ya nyumba katika jengo hilo kuwa 96.

“Changamoto yetu imekuwa ni mtaji ambapo tumekuwa tukiendelea kuzungumza na wawekezaji kwa ajili ya kuongeza mtaji.

“Kwa sasa tuna kitengo chetu cha ujenzi ambacho kimefika daraja la kwanza hatua itakayopunguza gharama za ujenzi na uuzaji wa nyumba zetu kwa ujumla. Pia, tuna malengo ya kuendelea kujenga nyumba kwenye halmashauri mpya ambapo halmashauri za Mbeya na Songea zimeonyesha nia ya kutaka kufanya kazi na sisi,” amesema Massawe.

Akizungumza na Mtanzania Digital kuhusu ukarabati huo mapema leo Machi 23, 2023 Afisa Uhusiano wa WHI, Maryjane Makawia amesema kuwa ujenzi ukarabati unaofanyika hivi sasa katika mradi huo wa Magomeni unatarajiwa kukamilika baada ya miezi Nane.

“Ni kweli tumeanza ujenzi wa kubadilisha matumizi ya vyumba nane tulivyokuwa tumetenga kwa ajili ya biashara ili kuwa nyumba, na hii ni baada ya agizo lililotolewa na mheshimiwa Waziri alipotembelea mradi wetu mwaka jana.

“Ujenzi huu unatekelezwa na sisi wenywe WHI na tunatarajia kuwa utachukua miezi nane kutoka sasa,” amesema Makawia.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
592,000SubscribersSubscribe

Latest Articles