27.2 C
Dar es Salaam
Friday, April 19, 2024

Contact us: [email protected]

WHI kutekeleza miradi mipya mitatu Dar

Na Faraja Masinde, Mtanzania Digital

Taasisi ya Nyumba ya Watumishi Housing Investment(WHI) inatarajia kuanzisha miradi mitatu ya ujenzi wa nyumba ndani ya Mkoa wa Dar es Salaam Kawe Apartment, Victory Apartment, Sea View Apartment ambayo itajengwa kwenye mkondo wa bahari karibu na hospitali ya Agha Khan hii yote ni nafasi kwa watanzania ambao wako tayari kununua hizo nyumba.

Hayo yamebainishwa Julai 6, 2022 na Meneja Mauzo wa WHI, David Mwaipaja kwenye wakati akizungumza na Mtanzania Digital katika Maonyesho ya 46 ya Biashara ya Kimataifa maarufu Sabasaba yanayoendelea jijini Dar es Salaam.

Amesema kukamilika kwa miradi hiyo kutatoa fursa kwa Watanzania wengi ambao watakuwa tayari kuweza kumilika nyumba hizo za kisasa.

“Baada ya miradi yetu ya wali kukamilika, kwasasa Watumishi Housing Investment tunatarajia kutambulisha miradi mipya mitatu ndani ya Jiji la Dar es Salaam, miradi hii ni pamoja na Kawe Apartment, Victory Apartment, Sea View Apartment ambayo itajengwa kwenye mkondo wa bahari karibu na hospitali ya Agha Khan, hivyo itakapokuwa tayari tutaitambulisha kwa Watanzania.

“Lengo la WHI ni kuhakikisha kuwa Watanzania wanapata makazi bora, hivyo kuhusu utaratibu wa malipo utakuwa ni uleule ambao umekuwa ukitumika katika miradi yetu iliyotangulia ikiwamo malipo endelevu ya kulipia nyumba kidogo kidogo wakati nyumba ikiwa kwenye ujenzi na pale nyumba itakapo kuwa imekamilika na akiwa amefikia hatua nzuri basi tutaangalia,” amesema Mwaipaja.

Aidha, amefafanua kuwa pamoja na kuuza nyumba hizo pia kuna fursa ya Watanzania kupanga kwenye nyumba hizo.

“Ndio maana utaona hata kwenye mradi wetu wa Gezaulole tumeanzisha nyumba za kupanga ili kusaidia wale ambao wanahitaji kupanga nyumba nzuri.

“Hivyo hata kwenye miradi mipya ya Kawe, Sea View au Victory itakuwa ni miradi mikubwa itakayohusisha majengo mengi kwani tuna nafasi kubwa.

“Miradi hii pia mbali nakuwa Dar es Salaam pia kuna mwingine Arusha na Dodoma ambako kuna mradi endelevu, hivyo niendelee kuwakaribisha Watanzania wote wafike kwenye banda letu hapa sabasaba au hata ofisini kwetu kwa ajili ya kupata maelezo namna ya kuweza kumiliki nyumba hizi.

“Tuko tayari kuhudumia Watanzania wote wa sekta ya umma na sekta binafsi, hivyo tupo kwa ajili ya kuhakikisha kuwa wanapata nyumba nzuri kwani tunajenga kwa ajili yao,” amesema Mwaipaja.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles