26.2 C
Dar es Salaam
Friday, December 3, 2021

WhatsApp yapunguza uwezo wa kusambaza ujumbe

Marekani

Mtandao wa kijamii wa WhatsApp umetangaza kupunguza uwezo wa wateja wake kusambaza ujumbe mara nyingi kutoka mara 20 hadi mara tano kwa siku.

WhatsApp, imesema uamuzi huo unalenga kupunguza usambazaji wa taarifa za uongo zinazosambazwa kupitia mitandao ya kijamii.

Uamuzi huo umetokana na kitisho kutoka kwa serikali ya India ya kuchukua hatua baada ya genge la watu kuwaua watu zaidi ya 20 wanaodaiwa kumteka mtoto na uhalifu mwingine uliosambaa kupitia ujumbe wa WhatsApp.

WhatsApp ilianzishwa mwaka 2009 na kisha kununuliwa na kampuni ya Facebook mwaka 2014, ambapo hadi kufikia mwanzoni mwa 2018 ilikuwa na zaidi ya watumiaji bilioni 1.5, ambao hubadilishana ujumbe bilioni 65 kwa siku.

- Advertisement -
bestbettingafrica

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

66,457FansLike
167,848FollowersFollow
526,000SubscribersSubscribe
- Advertisement -
10Bet

Latest Articles