27.2 C
Dar es Salaam
Wednesday, July 24, 2024

Contact us: [email protected]

WhatsApp inaweza kudukuliwa kupitia simu

WASHINGTON, MAREKANI

WADUKUZI wanaweza kuweka programu ya ‘software’ ya kuchunguza taarifa kwenye simu na vifaa vingine vinavyotumiwa kwa kutuma ujumbe wa WhatsApp, imethibitishwa.

WhatsApp ambayo inamilikiwa na Kampuni ya Facebook, imesema wanaodukua walilenga maeneo waliyochagua  ya watumiaji na walioongozwa na watumiaji wakuu wa mtandao.

Jumatatu wiki hii, WhatsApp iliwaomba watumiaji wake bilioni 1.5 kufungua upya app zao kama njia zaidi ya kuepuka udukuzi.

Shambulio hilo dhidi ya WhatsApp, lililogunduliwa mapema mwezi huu, lilikuwa ni la kwanza kuwahi kuripotiwa katika gazeti la Financial Times likiwahusisha wadukuzi wanaotumia sauti ya WhatsApp kuzipigia simu wanazozilenga.

Hata kama simu hizo hazitapokewa, tayari programu ya udukuzi huwa imewekwa ndani ya simu inayolengwa na mara moja ujumbe wa kumuonesha mwenye simu kuwa aliitwa na simu fulani hutoweka kwenye orodha ya simu zilizopigwa.

Kikosi cha usalama wa WhatsApp kilikuwa cha kwanza kubaini udukuzi huo, na kushirikisha taarifa hiyo makundi ya kutetea haki za binadamu, kampuni kadhaa za usalama na Wizara ya Sheria ya Marekani mapema mwezi huu.

“Wadukuzi wana kampuni binafsi ambayo inaripotiwa kufanya kazi na Serikali ambazo huwapatia mfumo wa udukuzi unaochukua udhibiti wa mfumo mzima wa simu,” WhatsApp iliwaambia wanahabari mapema wiki hii.

Imeripotiwa kuwa uvamizi huo wa mtandao wa WhatsApp ulibuniwa na kampuni ya usalama ya Israel inayofahamika kama NSO Group, ambayo awali ilielezewa kama “cyber arms dealer”.

Programu yake kuu ya software – Pegasus, ina uwezo wa kukusanya taarifa za siri kutoka kwa mlengwa, ikiwemo kuchukua data kwa kutumia kipaza sauti (microphone) na kamera na kukusanya taarifa za mahali alipo mtumiaji wa simu.

WhatsApp imesema ni mapema kujua ni watumiaji wangapi wameathiriwa na udukuzi huo, ingawa washukiwa wengi walilengwa kwa kiwango kikubwa.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
589,000SubscribersSubscribe

Latest Articles