23.3 C
Dar es Salaam
Saturday, April 20, 2024

Contact us: [email protected]

WFT wachambua sheria tano za uchaguzi

Na ASHA BANI-DAR ES SALAAM 

MTANDAO  wa Wanawake, Katiba, Uchaguzi na Uongozi, chini ya uratibu wa Mfuko wa Udhamini wa Wanawake Tanzania (WFT), umefanya uchambuzi wa sheria tano za uchaguzi kwa mrengo wa jinsia.

Kwa mujibu wa mtandao huo, malengo mahususi ya uchambuzi ni kutoa muhtasari wa mambo yaliyojitokeza kwenye baadhi ya sheria za uchaguzi ili kubainisha mapengo  yanayoweza kuwa kikwazo katika kutekeleza azma ya ujenzi wa demokrasia shirikishi kwa mrengo wa jinsia.  

Akizungumza kwa njia ya mtandao jana Mwenyekiti wa WFT, Profesa Ruth Meena alisema lengo la uchambuzi huo ni kutoa mapendekezo mahususi yatakayoongoza wadau mbalimbali katika kuchukua hatua stahiki zenye kukabiliana na sheria za ubaguzi wa aina zote, hususani ubaguzi wa jinsia kwenye mchakato wa uchaguzi. 

Alizitaja sheria zilizochambuliwa kuwa ni pamoja na Sheria ya Taifa ya Uchaguzi Sura ya 343 ya 2015, Sheria ya Uchaguzi ya Zanzibar namba 4 (2018), Sheria ya Uchaguzi wa Serikali za Mitaa namba 4 ya mwaka 1979 namba 292 kama ilivofanyiwa marekebisho mwaka 2010 na mwaka 2015, Sheria ya Serikali za Mitaa (Mamlaka za Wilaya Sura 287 kama ilivyorekebishwa 2002) na ile ya Serikali za Mitaa za Mamlaka za Miji sura ya 288 na Mamlaka za Wilaya sura ya 287. 

“Lengo la mkutano huu ni kuwezesha wanahabari kupata taarifa za kina zilizotokana na uchambuzi wa sheria zilizochambuliwa kwa mrengo wa jinsia. Kimantiki, wanahabari ni muhimu sana kwenye ujenzi wa demokrasia shirikishi na kwenye harakati za ukombozi wa wanawake kimapinduzi,” alisema Profesa Meena.

Alisema takwimu toka nchi nyingi zinazotumia mfumo huo zinaonyesha kwamba ufikiaji wa azma ya usawa wa jinsia ni mgumu.

Pia kwenye suala la haki ya kupiga kura, alisema katiba zote mbili ya Tanzania bara na visiwani zinabainisha haki sawa ya kupiga kura kwa raia wote wenye umri wa miaka 18 na kuendelea. 

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles