WFP yatangaza neema kwa wakulima wa Tanzania

0
857

Bethsheba Wambura, Dar es Salaam

Mkurugenzi Mkazi wa Shirika la Chakula Duniani (WFP) Michael Danford amesema wana mpango wa kuongeza ununuzi wa mazao hapa nchini na kuyapeleka katika nchi zenye uhitaji.

Akizungumza katika hafla ya utiaji saini wa mkataba wa makubaliano ya mauziano ya mahindi kati ya WFP na Wakala wa Taifa wa Hifadhi ya Chakula (NFRA) iliyofanyika Ikulu jijini Dar es Saalaam leo Ijumaa Januri 4, na kushuhudiwa na Rais Dk John Magufuli.

Amesema WFP imekuwa hapa nchini kwa takribani miaka 40 ikisaidia wakimbizi lakini wao kama shirika la kutoa chakula wameamua kuwasaidia wakulima amba ni wazalishaji wakuu wa bidhaa wanazohitaji.

“Kama mnavyofahamu WFP ndiyo inalisha wakimbizi wote waliopo hapa na tunasaidia hasa wanawake na watoto ili kuboresha lishe, hatutaki kile kinachotokea katika nchi zingine kitokee hapa’

“Tumeamua kufanya kazi kwa ukaribu na wzara ya kilimo ili kuwapa programu ambazo zitasaidia kuongeza ubunifu katika kilimo kwa wakulima wadogo haiwezekani katika nchi yenye asilimia 78 ya wakulima laini wanaochangia pato la taifa ni asilimia 30 lazima kuna pengo mahali, “ ameeleza Michael.

Aidha Michael amesema katika kupunguza gharama za usafirishaji wanafanya kazi kwa karibu na Shrika la Reli nchini (TRC) ili kutumia usafiri wa Treni kusafirisha chakula kwenda katika nchi jirani zenye uhitaji kwani njia hiyo ni rahisi na nafuu.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here