28.1 C
Dar es Salaam
Friday, October 11, 2024

Contact us: [email protected]

Weusi kuachia kazi mpya 

JENNIFER ULLEMBO-DAR ES SALAAM

WASANII wa kundi la Weusi wameanza kutimiza malengo yao ya kuhakikisha wanaachia kazi baada ya kazi mwaka huu.

Akizungumza jijini Dar es Salaam, mmoja wa wasanii wanaounda kundi hilo, John Makini ‘Joh Makini’, alisema walipanga kuingiza kazi mpya sokoni mapema wiki iliyopita.

Alisema sababu iliyowakwamisha ni msiba wa msanii Godzilla, hivyo tayari muda wowote kuanzia sasa wataachia kazi mpya.

“Tulipisha msiba wa msanii mwenzetu Godzilla, mashabiki wajiandae kusikia kazi yetu mpya tuliyoshirikiana na wasanii kutoka nchini Kenya,” alisema Joh Makini.

Joh Makini alisema wimbo wao umepewa jina la ‘Kutulia’, huku wakiwa wamewashirikisha Sautisol.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
590,000SubscribersSubscribe

Latest Articles