29.8 C
Dar es Salaam
Monday, October 7, 2024

Contact us: [email protected]

West Ham yampiga Arnautovic faini ya Sh milioni 594

LONDON, ENGLAND

KLABU ya West Ham imepanga kumtoza faini ya pauni 200,000 (sawa na Sh milioni 594 za Kitanzania) mshambuliaji wake, Marko Arnautovic, kwa kosa la kuonyesha utovu wa nidhamu.

Kutokana na sababu hiyo inayodaiwa ni kushinikiza uhamisho wake nchini China, nyota huyo aliondolewa katika kikosi kilichocheza dhidi ya  Bournemouth.

Arnautovic amesisitiza anataka  kuondoka mwezi huu  baada ya kujitokeza klabu ya  Shanghai SIPG inayocheza Ligi Kuu ya China, lakini West Ham imegoma kumuuza nyota huyo hadi watakapopata  mbadala wake.

Kwa mujibu wa gazeti la Daily Stars, uamuzi huo umeonekana kumwathiri mshambuliaji huyo baada ya Shanghai SIPG kuwa tayari kuweka mezani dau nono.

Kutokana na sababu hizo Kocha wa  West Ham, Manuel Pellegrini,  alimwondoa nyota huyo  katika kikosi chake kilichopangwa kucheza jana dhidi ya Bournemouth.

West Ham inadaiwa kuhitaji pauni milioni 45 baada ya kukataa ofa ya pauni milioni 35 kutoka Shanghai SIPG.

Pellegrini alisisitiza kuwa: “Arnautovic,  alifanya mazoezi wiki nzima bila tatizo lolote lakini ghafla alitoweka klabuni.”

Kutokana na kitendo hicho, Arnautovic  aliwaomba radhi wachezaji wenzake lakini hakuficha hisia zake kwamba anataka kuondoka jambo ambalo kocha wa timu hiyo  alitaka klabu hiyo kutafuta  mwarobaini wa tatizo hilo haraka.

Akizungumzia sakata la mchezaji huyo, Pellegrini alidai: “Marko ni mmoja kati ya wachezaji muhimu lakini vijana wangu wanafahamu kuwa kuna kitu kitatokea.”

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
590,000SubscribersSubscribe

Latest Articles