24.2 C
Dar es Salaam
Saturday, April 20, 2024

Contact us: [email protected]

Wesley Sneijder atundika daruga

AL GHARRAFA, QATAR

KIUNGO wa zamani wa Real Madrid na Inter Milan, Wesley Sneijder, ametangaza kustaafu soka huku akiwa na umri wa miaka 35.

Staa huyo wa zamani wa timu ya taifa ya Uholanzi, ametangaza kuachana na mara baada ya kumalizana na timu ambayo alikuwa anaitumikia Al-Gharafa SC inayoshiriki Ligi nchini Qatar.

Hata hivyo, mchezaji huyo kabla ya kutangaza kustaafu soka kulikuwa na taarifa kwamba amefanya mazungumzo na klabu ya Eredivisie side Utrecht kwa ajili ya kwenda kuitumikia, lakini amesitisha mpango huo.

“Nimekuwa na upendo wa hali ya juu kwenye mji huu, lakini sasa naomba niweke wazi kuwa, huu ni mwisho wangu wa kucheza soka la kulipwa, sasa ni wakati wa kuanza maisha yangu mapya nje ya soka.

“Haya ni maamuzi magumu kuyafanya hasa katika mchezo ambao unaupenda na umekufanya kuwa na jina kubwa duniani, lakini kila kitu kina mwisho wake, nadhani huu ni wakati sahihi wa kuwapisha wengine waendelee.

“Ninawashukuru sana mashabiki ambao walikuwa na mimi kwa kipindi changu chote cha maisha ya soka, nawashukuru wachezaji wenzangu pamoja na makocha kwa ushirikiano mkubwa, naishukuru fainali yangu kwa kunisapoti katika kila aina ya changamoto nilizopita, nawapenda sana,” alisema mchezaji huyo.

Sneijder alianza kucheza soka mwaka 2002 akiwa na klabu ya Ajax, ambapo alicheza jumla ya michezo 126 ya Ligi Kuu na kufanikiwa kupachika mabao 43, baada ya kuwa hapo hadi mwaka 2007 alipojiunga na Real Madrid na baadae kwenda Inter Milan, Galatasaray na Nice.

Alikuwa mmoja kati ya wachezaji wa Inter Milan waliotwaa mataji matatu katika msimu wa 2009/2010, wakichukua Ligi Kuu, Coppa Italia na Ligi ya Mabingwa chini ya kocha wa Jose Mourinho.

Hata hivyo, aliisaidia timu ya taifa ya Uholanzi kutinga fainali kwenye michuano ya Kombe la Dunia mwaka 2010 nchini Afrika Kusini, lakini walifungwa bao 1-0 dhidi ya Hispania.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles