29.8 C
Dar es Salaam
Sunday, September 15, 2024

Contact us: [email protected]

Wenye ulemavu wa ngozi waomba ulinzi

Na RENATHA KIPAKA

-Bukoba        

WATU wenye ualbino   Manispaa ya Bukoba, wameiomba Serikali wilayani humo kuwasaidia kuimarisha  ulinzi na katika kuelekea uchaguzi wa Serikali za Mitaa na Uchaguzi Mkuu mwaka 2020.

Walisema wakati wa uchaguzi, hulazimika kusimamisha shughuli za uzalishaji na kukaaa ndani kwa hofu ya usalama wa maisha yao.

Agusta Agustine, mkazi wa Kata ya Nshambya aliiambia Mtanzania kuwa huingiwa na hofu ya kupoteza maisha kutokana na kuripotiwa kwa matukio ya ukatili kwa watu wenye ulemevu huo.

 “Maisha ya hofu yanaingia   unaposikia sehemu nyingine ndani ya wilaya au nje ya mkoa mtu kama mimi amefanyiwa ukatili, kutolewa viungo kwenye mwili au kufa …jamani tupendane,” alisema Agustine.

Frolence Frolian mkazi wa  Mtaa wa Buyekera Kata Bakoba alisema wameamua kuomba msaada kwa Serikali kabla harakati za viongozi wanaogombewa nafasi hawajaanza kufanya kampeni.

 “Endapo viongozi wetu wa dini na wadau wakiingilia kati kutoa elimu kwa wanasiasa na waganga wa jadi, unyanyasaji na ukatili vitaondoka hasa  maeneo kama Ngara na nje ya mkoa kama Shinyanga,” alisema Frolian.

  Mrakibu   Mwandamizi wa Polisi Mkoa wa Kagera, Nsubisi Mwakisambwe, alisema ushirikishwaji wa jamii kwenye masuala ya matukio ya uhalifu na uvunjifu wa amani ni njia moja wapo ya kutatua changamoto.

Mwakisambwe alisema njia hiyo ni msaada pekee wa kujua usalama kwa kila hatua   inapooneka kuna hali yoyote katika mazingira ya wanajamii hasa.  

 Alisema  mikakati iliyopo ni kutambua idadi kamili ya watu hao na kuwapatia viongozi wa mitaa  ambao watakuwa washirIki zaidi katika ulinzi na usalama kwa kuitisha mikutano shirikishi ya kuwapa elimu wana jamii.

Naibu Meya wa Halmashauiri ya Manispaa ya Bukoba,  Jimmy Kalugendo, alisema wanasiasa ndiyo wamekuwa walengwa wa kudhaniwa ni watatafutaji kura kwa njia zisizokuwa  sahihi na hushirikiana na waganga wa jadi.

Alisema watambue kuwa upatikanaji wa kura siyo kwa kukatili maisha ya mwanadamu bali watumie kauri zao zenye kushawishi  wananchi kutoa kura kwa nia njema na ya amani na siyo kuondoa uhai wa mtu.

 “Nafasi ya uongozi inakuja kwa kujinadi  kwa wapiga kura na kuwatekelezea yale ambayo yanatakiwa na  sio vitendo vya ukatili vinavyotoolewa taarifa nyakati za uchaguzi.

“Nafasi nzuri ni matekelezo ya wananchi,” alisema Kalugendo.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
589,000SubscribersSubscribe

Latest Articles