33.2 C
Dar es Salaam
Friday, March 29, 2024

Contact us: [email protected]

WENGER: SIJUI NAONDOKA LINI ARSENAL

LONDON, ENGLAND


BAADA ya klabu ya Arsenal kufanikiwa kushinda mabao 5-0 dhidi ya Lincoh na kuingia hatua ya nusu fainali ya michuano ya Kombe la FA, kocha wa timu hiyo, Arsene Wenger, amedai hajui ataondoka lini ndani ya kikosi hicho.

Mbali na ushindi huo wa juzi, lakini bado mashabiki wa klabu hiyo wameendelea kuonesha nia ya kumtaka kocha huyo aondoke ndani ya kikosi hicho, lakini hali hiyo ilikuwa tofauti kidogo na ile ambayo mashabiki waliionesha kwenye mchezo dhidi ya Bayern Munich katika Ligi ya Mabingwa Ulaya.

Baada ya kutolewa kwenye michuano ya Ligi ya Mabingwa, Wenger alidai kuwa kelele za mashabiki haziwezi kumfanya afungashe mikoba yake na kuondoka, lakini ataweza kuondoka endapo watafikia makubaliano na uongozi wa timu hiyo.

Mkataba wa kocha huyo ndani ya kikosi hicho cha Arsenal unatarajiwa kufikia mwisho mara baada ya kumalizika kwa msimu huu wa ligi, lakini kocha huyo anadai kuwa hajui ni lini ataondoka.

“Nadhani nimekuwa nikionesha mapambano juu ya kuipigania klabu hii ya Arsenal, nitahakikisha ninafanya hivyo hata kama nitakuwa nje ya klabu hii, nimekuwa hapa kwa muda mrefu hivyo klabu ipo katika moyo wangu.

“Lengo langu ni kuendelea kuwa kocha wa klabu hii kwa muda mrefu, kila siku nimekuwa nikisema hivyo, lakini ukweli ni kwamba hadi sasa sijui nitakuwa ndani ya kikosi hiki kwa muda gani na sijui nitaondoka lini,” alisema Wenger.

Kocha huyo aliongeza kuwa  anajua mashabiki wapo katika wakati mgumu kutokana na matokeo yanayopatikana, lakini atapambana ili kuwapa furaha mashabiki hao ambao wamekuwa wakiandamana kila mara.

“Ninaangalia nini ninachokifanya katika kazi yangu, nawaacha wale ambao wamekuwa wakinijadili juu ya kazi yangu, wala sina wasiwasi na maneno yao, kikubwa ninachokiangalia ni jinsi gani nitashinda mchezo wangu ujao na kurudisha ubora wa timu,” aliongeza. 

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
585,000SubscribersSubscribe

Latest Articles