25.2 C
Dar es Salaam
Tuesday, April 23, 2024

Contact us: [email protected]

WENGER: NI KOSA LANGU ARSENAL KUFUNGWA NA LIVERPOOL

LONDON, ENGLAND


KOCHA wa klabu ya Arsenal, Arsene Wenger, amedai kuwa alaumiwe yeye kwa timu yake kuchezea kichapo cha mabao 3-1 dhidi ya Liverpool juzi kwenye michuano ya Ligi Kuu nchini England.

Mchezo huo uliopigwa kwenye uwanja wa Anfield, Arsenal walionekana kupoteana baada ya kufungwa bao la mapema katika dakika ya tisa ambalo liliwekwa wavuni na mshambuliaji wa Liverpool, Roberto Firmino, kabla ya bao la pili kufungwa na Sadio Mane katika dakika ya 40.

Timu hizo zilikwenda mapumziko huku wenyewe Liverpool wakiwa mbele kwa mabao 2-0, lakini baada ya kipindi cha pili kuanza, Arsenal walionekana kutafuta bao la mapema la kufutia machozi, waliweza kufanya hivyo katika dakika ya 57, ambalo liliwekwa wavuni na Danny Welbeck kabla ya Georginio Wijnaldum kuongeza bao la tatu kwa Liverpool.

Katika kikosi cha Arsenal, kocha wa klabu hiyo, Wenger, alimwacha mshambuliaji wake hatari ,Alexis Sanchez, huku kikosi chake kikichezea kichapo hicho, hivyo mashabiki wakaanza kumjia juu kwa mchezaji huyo kukaa benchi.

Sanchez amekuwa ni mshambuliaji ambaye anapachika mabao ndani ya kikosi hicho, hivyo Wenger anadai kuwa alifanya makosa kumwacha nje mchezaji huyo mwanzo wa mchezo huo na kusababisha kufungwa mchezo huo.

“Najua tulianza kuupoteza katika dakika 45 za kipindi cha kwanza, viungo walionekana kupoteana kwa kiasi kikubwa na ndio maana tuliupoteza mchezo huo, ukweli ni kwamba hatukuwa kwenye kiwango chetu.

“Ukiwa unatengeneza nafasi nyingi kuna uwezekano mkubwa ukashinda mchezo huo, lakini tulishindwa kufanya hivyo ila wenzetu waliweza kutengeneza nafasi na kuzitumia, hivyo ndivyo soka lilivyo.

“Kipindi cha pili tulionekana kuja kwa kasi na kutafuta mabao, kama tungefanya hivyo katika dakika 45 za kipindi cha kwanza, naamini tungefanikiwa kushinda mchezo huo. Napenda kusema kuwa, nilifanya makosa kumwacha Sanchez, huyu ni mchezaji ambaye anafanya vizuri katika safu ya ushambuliaji, lakini nilikuwa na mipango mingine ya kuusoma mchezo na ndio maana nilimwacha benchi na hali ikawa mbaya, nakubali kuwa ni kosa langu kumwacha mchezaji huyo,” alisema Wenger.

Kwa matokeo hayo, Arsenal imewafanya washike nafasi ya tano katika msimamo wa ligi na kutolewa kwenye ‘Top Four’, huku wakiwa na pointi 50 baada ya kucheza michezo 26, wakati huo vinara Chelsea wakiwa na pointi 63.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles