30 C
Dar es Salaam
Friday, January 27, 2023

Contact us: [email protected]

WENGER: NAKARIBIA KUTOA TAMKO LA UWEPO WANGU ARSENAL

LONDON, ENGLAND


BAADA ya klabu ya Arsenal kukubali kipigo cha mabao 3-1 juzi dhidi ya West Brom, Kocha wa timu hiyo, Arsene Wenger, ameweka wazi kuwa tayari amefanya maamuzi yake na anatarajia kuyatangaza muda mfupi ujao.

Kocha huyo kwa sasa amekuwa na wakati mgumu ndani ya Emirates, kutokana na mashabiki kuandamana mara kwa mara wakidai kocha huyo aondoke baada ya kushindwa kuleta mataji kwa muda mrefu.

Japokuwa mashabiki hao wamekuwa na mabango mara kwa mara, lakini kocha huyo hajaweka wazi kuwa ataondoka au ataendelea kukaa, lakini amedai tayari amefikia kufanya maamuzi ambayo anaweza kuyasema hata kabla ya msimu kumalizika.

Mbali na kukosa mataji kwa muda mrefu, lakini kocha huyo tangu ameichukua timu hiyo miaka 20 iliyopita imekuwa ikiingia ‘Top Four’ na kushiriki Ligi ya Mabingwa barani Ulaya, tofauti na klabu nyingine, lakini mashabiki wamedai kushiriki Ligi ya Mabingwa si tatizo, kikubwa wanachokiangalia ni kutwaa taji la Ligi.

Katika michezo tisa ambayo Arsenal imecheza, imeweza kupoteza michezo sita, wakati huo katika michezo mitano ya Ligi Kuu iliyocheza siku za hivi karibuni imeweza kupoteza, ila Wenger amewataka mashabiki wasiwe na wasiwasi atatoa tamko.

“Ondoeni wasiwasi, najua nini nataka kukifanya kwa wakati ujao ndani ya klabu hii, kila mmoja atajua ni siku za hivi karibuni, lakini kwa sasa siwezi kusema hayo mara baada ya kupoteza mchezo dhidi ya West Brom, najua ninachokifanya.

“Hata hivyo, maamuzi hayo siwezi kuyaweka wazi wakati wa michuano ya kimataifa, najua kwamba nipo katika kipindi kigumu kwa maisha yangu ya miaka 20 ambayo nimekaa ndani ya klabu hii.

“Kikubwa ambacho kipo kwa sasa ni kutokana na kupoteza michezo mara kwa mara, lakini ninachokiangalia ni jinsi gani tutaweza kupambana ili kurudisha ubora wa timu, kuwania nafasi ya kushiriki michuano ya Ligi ya Mabingwa Ulaya, hilo ni jambo muhimu sana kwangu.

“Hakuna njia nyingine ya kufanya zaidi ya kupambana kwa kila namna hadi siku ya mwisho na tusipofanya hivyo, tutakuwa katika wakati mgumu sana na kama tutashindwa kuingia top four basi wapo ambao watafurahia hali hiyo,” alisema Wenger.

Hata hivyo, kuna taarifa kwamba, kocha huyo baada ya wiki mbili zijazo anaweza kuongeza mkataba wa miaka mwili, japokuwa mashabiki hawamtaki, hivyo uongozi upo katika mazungumzo na mteja wao na wanaweza wasikubaliane.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
208,063FollowersFollow
561,000SubscribersSubscribe

Latest Articles