27.7 C
Dar es Salaam
Saturday, June 10, 2023

Contact us: [email protected]

WENGER: AUBAMEYANG NA MKHITARYAN WANAHITAJI MUDA

LONDON, ENGLAND

KOCHA wa Arsenal, Arsene Wenger, amesema wachezaji wapya wa timu hiyo,

Henrikh Mkhitaryan na Pierre-Emerick Aubameyang, wanahitaji muda kabla ya kuanza kuonesha ubora wao na kuisaidia timu hiyo.

Wachezaji hao ambao wamesajiliwa katika dirisha dogo la Januari mwaka huu kutoka Manchester United na Borrusia Dortmund, walionekana kuwa na msaada mkubwa wakati Arsenal ikipata ushindi wa mabao 5-1 dhidi ya Everton hivi karibuni.

Matokeo mabaya baada ya mchezo huo yamemfanya Aubameyang kushindwa kuwa na msaada na kujikuta akipata bao moja katika michezo minne aliyocheza.

Hali hiyo inafanana pia na Mkhitaryan ambaye ameshindwa kufanya vizuri baada ya mchezo huo.

Mkhitaryan na Aubameyang pia  wameonekana kushindwa kuizuia Manchester City kutamba mbele yao baada ya Arsenal kufungwa mabao 3-0 katika mchezo wao wa pili baada ya kupita siku tano walipokutana katika fainali ya Carabao na kufungwa mabao 3-0.

Katika mchezo huo raia huyo wa Gabon alikosa penalti baada ya kuokolewa na kipa wa Manchester City, Ederson Moraes.

Lakini Wenger anaamini Januari ni mwezi mgumu kusajili mchezaji na kufanya vizuri, hata hivyo anajipa matumaini kuwa wachezaji hao watafanya vizuri baadaye.

“Wanahitaji muda wa ziada kuzoea mazingira,” alisema Wenger baada ya kipigo cha mabao 3-0 walichokipata kutoka kwa Manchester City juzi.

“Mambo yanabadilika haraka sana. Ni sehemu ya mchezo wa soka, siku hizi ukipoteza mchezo mmoja unakuwa katika presha, lakini wachezaji waliojiunga na Arsenal hivi karibuni watafanya vizuri siku zijazo,” alisema Wenger.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
213,414FollowersFollow
568,000SubscribersSubscribe

Latest Articles