22.9 C
Dar es Salaam
Monday, September 9, 2024

Contact us: [email protected]

Wenger amtaka Henry kuacha uchambuzi

 Thierry Henry akiwa na Arsene Wenger
Thierry Henry akiwa na Arsene Wenger

 

London, England

Kocha wa Klabu ya Arsenal, Arsene Wenger, amemtaka mchezaji wake wa zamani, Thierry Henry, kuchagua moja kati ya kuendelea kuwa kocha au mchambuzi wa soka.

Henry kwa sasa ni kocha wa vijana wa Arsenal, pia ni mchambuzi wa soka katika kituo cha utangazaji cha Sky Sports nchini England.

Wenger anamshangaa Henry kufanya kazi ya kufundisha na baadaye kwenda kukosoa.

Kocha huyo mwenye umri wa miaka 66, amedai kwamba haina maana kutumia siku zote kufundisha timu, kisha ikifika mwishoni mwa wiki anakaa kwenye runinga na kuanza kuwakosoa wachezaji.

“Hakuna sababu ya kuendelea kuwa kocha, huku baada ya kuwafundisha wachezaji unakwenda kuwakosoa kwenye uchambuzi, Henry anatakiwa kuchagua moja, kati ya uchambuzi na ukocha, ni bora aendelee na ukocha kwa kuwa wachezaji wengi wanatamani kufika alikofika.

“Lakini sidhani kama kuna watakaotamani kufanya kile ambacho anakifanya sasa katika uchambuzi wake,” alisema Wenger.

Henry analipwa na kituo hicho cha utangazaji pauni milioni 4 kwa mwaka, hivyo anaamini hata kama akiendelea kuwa katika klabu hiyo ya Arsenal hawezi kulipwa fedha hizo zote zaidi ya kugawana na viongozi wengine atakaokuwa nao.

Hata hivyo, kauli ya Wenger inaonekana kumgusa Henry ambaye amedai anaweza kutafuta klabu nyingine ya kufundisha kama maneno ya kocha huyo yakiendelea.

Inadaiwa kwamba Wenger alianza kupishana kauli na Henry baada ya kueleza katika uchambuzi wake, kuwa Olivier Giroud hatoshi kuongoza safu ya ushambuliaji ya Arsenal.

Hivyo, Henry alimtaka Wenger kufanya mipango ya kusajili mshambuliaji mwingine ili kuongeza nguvu, kauli ambayo ilionekana kama kumkosoa kocha huyo.

Katika hatua nyingine, Arsenal inatarajia kumwongezea mkataba Wenger kufuatia taarifa kuwa anawaniwa na timu ya taifa ya England kuchukua nafasi ya Roy Hodgson aliyejiuzulu baada ya kutolewa kwenye michuano ya Euro 2016.

Hata hivyo, Wenger alikanusha uvumi huo akisema hana mpango wa kuifundisha timu hiyo na kwamba ataendelea kuinoa Arsenal.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
589,000SubscribersSubscribe

Latest Articles