33.2 C
Dar es Salaam
Friday, March 29, 2024

Contact us: [email protected]

WEMA: USTAA NI MATESO, NIACHENI

Na KYALAA SEHEYE

“NAHITAJI kupumzika sasa, nimechoka kuhusishwa na mambo yasiyo na mashiko. Kwakweli nimechoshwa na ninaumizwa sana na hii hali,” ndivyo anavyosema msanii wa filamu za Kibongo, Wema Sepetu.

Wema ambaye ni Miss Tanzania mwaka 2006, amezua mjadala mkubwa kwenye mitandao ya kijamii baada ya clip inayosikika sauti inayodaiwa ni yake akizungumza kimahaba na mtu anayedaiwa kuwa ni Freeman Mbowe, Mbunge wa Hai na Mwenyekiti wa Chadema, taifa.

Katika clip hiyo iliyoanza kusambaa kwa kasi tangu wikiendi iliyopita, sauti inayodaiwa kuwa ni ya Wema na ile inayoelezwa ni ya Mbowe, wanazungumza katika hali ya mahaba huku wakionekana kuwa kwenye uhusiano wa kimapenzi.

Mwanamume kwenye clip hiyo (anayedaiwa kuwa ni Mbowe), anajaribu kumuomba msamaha mwanamke (anayedhaniwa kuwa ni Wema) na kumtaka aende Kilimanjaro kwa mazungumzo zaidi katika siku za mwisho wa wiki.

Tayari Mbowe ameshakanusha vikali kuwa sauti ile siyo yake, bila kufafanua zaidi, akitaka muda uachwe uzungumze kwa vile suala hilo linafanyiwa kazi kwa upande wao.

Wema ameibuka na kueleza masikito yake kwa kuhusishwa katika clip hiyo akidai kuwa anaumizwa na namna watu wanavyomfuatafuata na kumchafulia jina lake.

Wema ameliambia Swaggaz kuwa, amekuwa akijitahidi sana kukaa mbali na vyombo vya habari ili asiripotiwe vibaya lakini anaona haisaidii.

“Nimeamua nikae mbali na mitandao, nitulie nifanye mambo yangu lakini naona haisadiii. Siyo siri nimechoshwa na hii hali, natamani atokee staa mwingine abebe huu mzigo nami nipumzike ili niweze kufanya majukumu yangu niliyonayo.

“Nafahamu Watanzania wana shida nyingi, nami nimejipanga kuwa mtetezi wao hasa wanawake na wasichana kwa ujumla.

“Nimejitahidi kukaa kimya kwa muda mrefu na kupotea  kwenye mitandao ni  na sehemu za starehe kwa kujichimbia nikifanya mambo yangu na kutafakari namna ambayo nitakitumikia chama changu (Chadema) lakini binadamu bado wameendelea kuniandama ili wapate cha kuniongelea,” anasema Wema na kuongeza:

“Kweli kabisa… huu ustaa sasa naona ni mzigo kwangu. Natamani atokee msichana mwingine awe staa kunizidi ili na yeye aandikwe sasa. Kila siku Wema, why? Nakwazika sana kwa kweli.”

 

KINACHOMKERA ZAIDI

Wema anasema anachukizwa sana na tabia ya kuzushiwa mambo, kwani anaweza kuwa karibu hata na ndugu yake, akazushiwa ni mpenzi wake.

“Nakerwa mno ninapokuwa na mwanamume karibu hata kikazi nasingiziwa kuwa ni mpenzi wangu, hii ni kero. Naomba nisionekane mwanamke wa kila mtu, sasa niheshimiwe kama wengine wanavyoheshimiwa.

“Ninapokuwa karibu na mtu wa jinsia nyingine nisifikiriwe kutoka naye kimapenzi, kwa kuwa kuna watu ninawaheshimu kama Mwenyekiti…

“Hii imeniumiza hadi nilitamani kuachana na siasa ila mama yangu, ndugu zangu na Mwenyekiti mwenyewe wamenipa moyo na hapo ndipo nimepata nguvu za kufanya kazi kwa nguvu kuliko hapo awali,” anasema Wema.

 

AFAFANUA KUHUSU CLIP

“Sina uhakika kama ni sauti yangu kwa kuwa sikumbuki siku wala saa niliyoongea maneno hayo, hivyo kazi hiyo naiacha chini ya Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania ‘TCRA’ ili kubaini ukweli wa jambo hili.

“Kwa sasa sihitaji kuhusika wala kuliongelea kwa kina, nina uhakika ukweli utajulikana na sheria itachukua mkondo wake,” anasema Wema.

 

MIKAKATI YAKE

“Kwa sasa mikakati yangu ni kukitumikia chama changu kwa kuleta wanachama wengi zaidi kuhakikisha uchaguzi ujao kinafanya vizuri na kushinda ushindi wa kishindo.

“Hilo wapinzani wangu wanalijua na ndiyo maana wanatafuta skendo zisizo na maana ili kunirudisha nyuma ila ndiyo wamenipa nguvu ya kufanya kazi kwa kasi na kuniweka katika nafasi ya kujua siasa ni mchezo wa aina gani,” anasema.

 

MALENGO YAKE

“Malengo yangu ni kuwa kiongozi na hilo linajulikana kwa sababu uwezo ninao, nia ninayo na nguvu za kuwatumikia wananchi ninazo hivyo siasa zao za majitaka kwangu hazitakuwa na nafasi.

“Kama walikuwa wanajua Wema ni yule wa zamani, wa kukwazwa na vitu visivyo na msingi hilo wamenoa. Wema huyu ni kamanda ambaye anajiamini na kujitambua na nitasimama kutetea haki za wanyonge kama ilivyo sera ya chama changu,” anasema.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
585,000SubscribersSubscribe

Latest Articles