25.1 C
Dar es Salaam
Saturday, December 9, 2023

Contact us: [email protected]

WEMA, SHILOLE MNAVUNA MLICHOPANDA

NA MWANDISHI WETU

WIKI hii staa wa filamu za Tanzania na Miss Tanzania mwaka 2006, Wema Sepetu, aliweka wazi hisia zake za kuteswa na yanayoendelea mitandaoni kwa watu kumtukana matusi ya nguoni kiasi cha kutamani muumba wake amtoe uhai.

Mrembo huyo mwenye wafuasi wengi  zaidi nchini, alitishia kujitoa kwenye mtandao wa Instagram, baada ya kupata matusi na kejeli, huku watukanaji wengine wakimhusisha mama yake mzazi, jambo linalofanya ajutie kuwa maarufu.

Ukiachana na Wema, msanii wa Bongo Fleva, Zuwena Mohamed ‘Shilole’ naye amegonga vichwa vya habari za burudani baada ya kile kinachosemekana penzi lake na mchumba wake, Ashrafu Uchebe, kuingia doa.

Wawili hao wamethibitisha kuwa hali si shwari na kuna kitu kama ugomvi kinaendelea kati yao kiasi cha mchumba wake huyo kumwomba msamaha Shilole na Shilole kumsamehe, huku akimwambia, misukosuko kwenye mapenzi ni kawaida, hivyo inabidi wavumiliane.

Shilole na mchumba wake huyo ambaye anatarajia kumwoa Desemba 20, mwaka huu, waligonga vichwa vya habari baada ya picha za Shilole akiwa na mpenzi wa zamani, Nuh Mziwanda, kuvuja, hali iliyovuruga mawasiliano na mchumba wake.

Tukio la Wema na hili la Shilole ni matukio tofauti, lakini yaliyosababishwa na kitu kimoja tu. Wameshindwa kutenganisha maisha yao halisi na yale ya umaarufu kiasi cha ustaa kuathiri maisha yao ya kawaida.

Wema Sepetu amekuwa akianika maisha yake binafsi, hasa ya mapenzi hadharani, suala ambalo limempa shida muda wote wa miaka 11 ya umaarufu wake. Sidhani kama angeweka siri kwenye ishu zake za mapenzi leo angejuta kuwa staa.

Mbona tunaona wasichana wengi maarufu hawaweki hadharani maisha yao binafsi na wanajijengea heshima kubwa kutokana na kazi zao, Wema anashindwa nini? Lazima ajitafakari.

Hali kadhalika, Shilole, ambaye naye amekuwa akiweka hadharani maisha yake binafsi, leo hii anahangaika kunusuru uchumba wake na kila mtu anafahamu jambo ambalo ilitakiwa alifanye siri kwa sababu haliwahusu mashabiki wa muziki wake.

Hivyo basi, matatizo ambayo warembo hawa (Wema na Shilole) wanapitia, ni matunda halisi waliyoyapanda wenyewe kwa kuanika maisha yao binafsi katika hadhara ya mashabiki.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
580,000SubscribersSubscribe

Latest Articles