30.2 C
Dar es Salaam
Tuesday, August 9, 2022

WEMA SEPETU USIPOLINDA JINA LAKO NANI ALILINDE?

NA CHRISTOPHER MSEKENA

SI jambo rahisi kwa staa kudumu kwenye kilele cha umaarufu kwa miaka 10 mfululizo na mashabiki wakaendelea kukupenda na kukupa ushirikiano ule ule. Hii hutokea mara chache, kwani mastaa wengi hushindwa kusimamia vile vitu vinavyowapa ustaa kiasi kwamba baada ya muda mfupi hupotea kwenye ramani.

Hapa Bongo tuna mastaa wachache wenye kaliba hiyo, ambapo miongoni mwao ni Miss Tanzania mwaka 2006, Wema Sepetu, ambaye toka alipolitwaa taji hilo mpaka leo hii ana miaka 11, lakini ustaa wake haujawahi kushuka, kila siku unapanda.

Hata pale alipoamua kutumia talanta yake nyingine ya uigizaji hadhi yake ilizidi kuongezeka, kwani mashabiki wengi tulifurahi kuona upande mwingine wa mrembo huyo ndani ya filamu za Kibongo. Kama ulikuwa hufahamu kwa mastaa wa kike, Sepetu anaongoza kuwa na wafuasi wengi kwenye mtandao wa Instagram na Afrika Mashariki ni wa pili, akifuata nyayo za Lupita Nyong’o.

Wema ana wafuasi milioni 3.1, huku Lupita wa Kenya akiwa na watu milioni 4.2, hivyo mrembo huyu si wa mchezo, ana umaarufu uliotokana na heshima iliyojengwa kwa vitu vidogo vidogo toka alipotawazwa kuwa Miss Tanzania.

Lakini jambo la kushangaza ni kwamba, Wema amekuwa haonekani kwenye matangazo ya kampuni kubwa akinadi bidhaa au akiwa balozi wa kampuni fulani kama tunavyoona kina Flaviana Matata, Milen Magese, Ali Kiba na Diamond Platnumz.

Tatizo ni nini? Hilo ni swali ambalo nadhani hata yeye mwenyewe Wema anapaswa kujiuliza, kwani mashabiki anao wa kutosha, hali kadhalika ni mtu mwenye ushawishi na mvuto mkubwa, lakini kwanini hapati dili za kutangaza bidhaa au zile za kibalozi?

Hakuna kitu kingine zaidi ya namna ambavyo Wema anashindwa kulilinda jina lake, anashindwa kupambana ili kuhakikisha maisha yake binafsi hayaharibu wadhifa wake kiasi cha kuwakimbiza wawekezaji, anapaswa kutambua kuwa, jina lake ndiyo biashara yake, hivyo anapaswa kuacha mambo yanayolibomoa jina lake.

Mfano ni mwaka jana, picha zake za faragha akiwa na mwanamitindo Calisah zilivuja, hali kadhalika wiki hii picha kama hizo hizo zimesambaa mitandaoni, ni vitu hivi vinavyomtia doa mrembo huyu na kufanya aonekane hajakua na hajatambua kuwa ana jukumu la kulilinda jina lake kadri awezavyo.

 

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
198,291FollowersFollow
550,000SubscribersSubscribe

Latest Articles