WEMA SEPETU KUSOMEWA MAELEZO YA AWALI JULAI

0
723
Wema Sepetu

Na PATRICIA KIMELEMETA

MAHAKAMA ya Hakimu Mkazi Kisutu, inatarajia kumsomea maelezo ya awali msanii Wema Sepetu na wenzake wawili, Julai 10, mwaka huu kwenye kesi inayowakabili ya kukutwa na msokoto mmoja na vipisi vya bangi vyenye uzito wa gramu 1.08.

Wema na wenzake, Angelina Msigwa na Matrida Abas walifikishwa mahakamani hapo wakikabiliwa na makosa mawili likiwamo la kukutwa na kiasi kidogo cha dawa za kulevya.

Wakili wa Serikali, Elizabeth Mkunde, alidai mahakamani hapo jana mbele ya Hakimu Godfrey Mwambapa kuwa, upelelezi wa kesi hiyo umekamilika na kuiomba mahakama hiyo kupanga tarehe nyingine kwa ajili ya kuwasomea maelezo ya awali.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here