27 C
Dar es Salaam
Friday, May 27, 2022

Wema Sepetu afunguka penzi la siri linavyompa raha

 BEATRICE KAIZA

MARA kadhaa tumeona mastaa wanapofika kwenye vilele vya umaarufu kinachofuata ni kuanguka au kupoteza kabisa nafasi walizonazo, ila sio kwa Wema Sepetu a.k.a Tanzania Sweetheart.

Mrembo huyo amefanikiwa kubaki katika kilele cha umaarufu tangu alipoukwaa ustaa kwenye mashindano ya urembo 2006, kisha kujitupa kwenye uingizaji anaoufanya kwa mafanikio mpaka sasa.

Juzi kati aliibuka na kipindi chake, Cook With Wema Sepetu kinachopatikana kwenye App na chaneli yake ya YouTube japo kuwa hata akiwa kimya, jina lake halijawahi kukauka kwenye midomo ya wajumbe (mashabiki).

Alhamisi wiki hii, Wema Sepetu alitangaza kurudi upya kwenye ulimwengu wa filamu akiwa mhusika mkuu katika tamthilia mpya ya Karma, inayoanza kuruka leo kupitia chaneli ya Maisha Magic Bongo (DSTV).

Baada ya kufanya mazungumzo na vyombo vya habari jijini Dar es Salaam, Swaggaz tulimvuta pembeni na kuzungumza naye mengi kuhusu kazi na maisha yake binafsi yanayowavutia mashabiki wengi.

Swaggaz: Hujaonekana kwa muda mrefu kwenye filamu, umekuja na zawadi gani kwa mashabiki?

Wema Sepetu: Kwa sasa nitakuwa naonekana kwenye tamthilia ya Karma ambayo itakuwa inaonekana kila siku za Jumamosi na Jumapili kwa saa nzima kuanzia kesho kutwa (leo).

Swaggaz: Karma ni tamthilia yenye maudhui gani?

Wema Sepetu: Kwenye Karma ni tamthilia yenye uhondo wa kusisimua, ndani yake kuna siasa, pesa, visasi na mapenzi, ndio vitu vinne tunavyokwenda kushuhudia kwenye tamthilia hii ambayo inakuja kukonga nyoyo za wapenzi wangu.

Na Karma ni neno la kituruki lenye maana ya utu na kama utafanya ubaya utalipwa kwa ubaya siwezi kuongea sana mashabiki zangu wakae karibu na Dstv ili kujionea wenyewe uhondo wa tamthilia hii.

Swaggaz: Unafanya kazi na wanamitindo wengi ila kwanini ukitengenezewa vazi na Martin Kadinda huwa anafunika zaidi?

Wema Sepetu: (anacheka) Yaani Martin ni kila kitu kwangu kwenye mambo ya mavazi na hajawahi kukosea ndio maana akinitengenezea nguo lazima nifunike.

Mfano ni siku ile ya uzinduzi wa EP ya Zuchu nilishangaa wengi walinipongeza kwa kupendeza, inatokea tuu, si unajua watu na nyota zetu, huwezi kuamini kuwa hata nguo zilikuja nikiwa ‘location’ na nilizivalia nikiwa huko huko, binafsi sijawahi kupania sherehe jamani.

Swaggaz: Na kwanini hivi karibuni umekuwa ukipenda zaidi pendeza kwa kuvaa mavazi meupe?

Wema Sepetu: Na bado watu watengemee kuniona na nguo nyeupe tena na tena, nimejikuta tu napenda rangi hii nyeupe kwa sababu nimeona inanipendeza na kwa ushauri ambayo Kadinda ananipa.

Swaggaz: Ulipokuwa mnene ulikuwa huonekani kwenye uigizaji ila ulipopungua umepata nafasi ya kuigiza tamthilia mbili mfululizo, We Men na Karma, je wembamba ndio siri ya mafanikio yake kwenye uigizaji kwa kwasa?

Wema Sepetu: Ndio, yaani sasa hivi ni kazi kwenda mbele, nafanya kipindi changu cha Cook With Wema Sepetu, matangazo ya biashara, tamthilia nk, kila kitu nafanya kwa sababu najiona mwepesi na ninaupenda sana mwili wangu wa sasa.

Swaggaz: Umebadilika kwa kuweka usiri mahusiano yako ya mapenzi, unaifurahia hiyo hali?

Wema Sepetu: Nayafurahia sana mapenzi yangu ya sasa ya kuweka ‘private’ mahusiano, ni watu wachache ndio wanamjua mpenzi wangu hadi pale ambapo nitaolewa na ni hivi karibuni tu, Inshallah.

Swaggaz: Haya mama asante kwa muda wako.

Wema Sepetu: Thank you, shukrani.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
192,454FollowersFollow
541,000SubscribersSubscribe

Latest Articles