28.6 C
Dar es Salaam
Saturday, January 28, 2023

Contact us: [email protected]

WEMA SEPETU AENDELEA KUSOTA RUMANDE

Na PATRICIA KIMELEMETA-DAR ES SALAAM

MWIGIZAJI wa filamu nchini ambaye pia ni Miss Tanzania 2006, Wema Sepetu, ameendelea kusota rumande tangu alipokamatwa na Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam, Februari 3, mwaka huu akidaiwa kukutwa na bangi.

Wema ni miongoni mwa wasanii 13 waliotajwa na Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda ambao walitakiwa kukutana naye Kituo Kikuu cha Polisi Dar es Salaam kwa mahojiano, kutokana na kudaiwa kujihusisha na utumiaji wa dawa za kulevya.

Wema anashikiliwa na polisi kituoni hapo tangu alipokwenda kwa mahojiano na baada ya uchunguzi wake kukamilika atafikishwa mahakamani kujibu tuhuma zinazomkabili.

Hata hivyo, Kamanda wa Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam, Simon Sirro alidai kuwa baada ya kufanya msako nyumbani kwa msanii huyo, walikuta kete mbili za bangi na karatasi za kusokotea.

“Tulifanya msako nyumbani kwake na tukakuta kete mbili za bangi na karatasi za msokoto na bado tunaendelea na mahojiano naye tukimaliza tutamfikisha mahakamani,’’ alisema Kamanda Sirro.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
208,063FollowersFollow
561,000SubscribersSubscribe

Latest Articles