Wema awapa onyo wasanii

0
541

Na GLORY MLAY

STAA wa filamu nchini na Miss Tanzania mwaka 2006, Wema Sepetu amesema si jambo la kiungwana lwa wasanii kutomheshimu shabiki wake kwa kuwa bila hao hawawezi kuwa msanii.

Akizungumza na MTANZANIA jana, Wema, alisema kuwa mashabiki ndio watu ambao wanaweza kumapa msanii ushauri kuhusiana na kazio zake kwani wao ndio wanaozinunua hivyo waheshimiwe.

“Kuna baadhi ya wasanii wanatumia majina yao vibaya, ukiwa staa unatakiwa uwe ‘smart’ ujipende, uwe na upendo na wenzako, uwe mvumilivu unayejiheshimu na kuheshimu watu wako wakiwamo mashabiki.

“Mashabiki wanatufanya tuwepo hapa mjini na tunaishi vizuri kwasababu wao wananunua kazi zetu, hivyo ninawaomba wasanii wasijibizane na mashabiki wala kuwadharau,” alisema.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here