25.1 C
Dar es Salaam
Saturday, December 9, 2023

Contact us: [email protected]

Wema atoka mahabusu, Hakimu amuonya

Kulwa Mzee, Dar es Salaam

Msanii wa Filamu nchini, Wema Sepetu aliyekuwa mahabusu katika Gereza la Segerea ameachiwa kwa onyo na dhamana yake inaendelea.

Uamuzi huo umetolewa leo Jumatatu Juni 24, saa nne asubuhi katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu mbele ya Hakimu Mkazi, Maira Kasonde.

Akitoa uamuzi wa aidha Wema afutiwe dhamana au la, Hakimu Kasonde amesema kazingatia kiapo kilichowasilishwa na Wakili Albert Msando na maelekezo ya mshtakiwa lakini mahakama inaona ni kweli alivunja masharti ya dhamana.

Amesema sababu kubwa ni kuumwa ghafla ambapo alitakiwa siku ile ile angefika mahakamani kutoa taarifa si kuamua kuondoka.

“Mahakama inakuonya, uhakikishe pale ambapo haupo mahakamani, Mahakama ijulishwe kupitia mdhamini wako na si vinginevyo,” amesema Hakimu Kasonde.

Hakimu Kasonde amesema kosa hilo likijirudia Mahakama haitasita kumfutia dhamana.

Wema alienda gerezani Juni 17 mwaka huu, ambapo anakabiliwa na mashtaka ya kusambaza video ya ngono katika mitandao ya kijamii kupitia simu yake ya kiganjani.

Juni 11 mwaka huu  Mahakama ilitoa hati ya kumkamata Wema kwa kosa la kuruka dhamana.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
580,000SubscribersSubscribe

Latest Articles