27.2 C
Dar es Salaam
Monday, March 20, 2023

Contact us: [email protected]

Wema atoa dili kwa wadau wa filamu

NA BRIGHITER MASAKI

MSANII wa Filamu nchini, Wema Sepetu, baada ya kuwa kimya kwa muda mrefu kwenye filamu, amekuja na kutoa dili kwa wadau 150 wa filamu.

Msanii huyo ameamua kufungua kampuni yake mpya ambayo inajulikana kwa jina la ‘Wema Sepetu Empire’ kwa ajili ya kuinua wasanii wachanga na wasanii hao wataonekana kwenye tamhilia yake mpya, Agosti mwaka huu.

Mbali na kutoa dili hilo, lakini msanii huyo ameweka wazi kuwa, tayari kampuni hiyo imetoa ajira kwa wasanii wachanga wasiopungua 60 baada ya kufanya usahili mwishoni mwa wiki iliopita katika viwanja vya Leaders jijini Dar es salaam.

“Washindi waliopatikana watakuwa chini ya Wema Sepetu Empire, hii ni kampuni ambayo ipo chini ya Endless Fame inayosimamia filamu zangu kwa muda mrefu, Siku zote naamini katika kula na wenzangu na kutokuwa mchoyo kwa kuwa mimi nilishikwa mkono na marehemu Steven Kanumba.

“Hivyo na mimi natakiwa kuwa na zao langu kwa jamii inayonizunguka na ninaamini kuna wasanii wengi wenye vipaji mtaani, lakini hajapata sapoti,” alisema Wema.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
210,784FollowersFollow
563,000SubscribersSubscribe

Latest Articles