25.9 C
Dar es Salaam
Wednesday, December 1, 2021

Waziri Zungu asisitiza matumizi nishati mbadala

Mwandishi Wetu – Dar es Salaam

WAZIRI wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira),  Mussa Zungu amezungumzia umuhimu  wa matumizi ya  nishati mbadala ya gesi ambayo ni rafiki kwa mazingira ukilinganisha na mkaa na kuwataka watanzania kugeukia matumizi ya gesi ili kulinda mazingira.

Akizungumza na waandishi wa habari juzi jijini Dar es Salaam, baada ya kufanya mazungumzo na Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Circle Gas, Volker Schultz,  alisema kuwa elimu na uhamasishaji zaidi unahitajika kuhusu matumizi mbadala ya nishati.

“Tanzania kama nchi ina hamasisha matumizi ya nishati mbadala kama suluhisho pekee la kulinda misitu na mazingira kwa ujumla. Tumekua tukichukua hatua mbalimbali kushirikiana na wadau wa mazingira,” alisema.

Alisema Schultz alimtembelea kumwelezea mpango wa kampuni yake kuhamasisha matumizi  ya gesi katika majiji ili kupunguza ukataji miti hovyo ambao umekuwa  ukiathiri mazingira.

“Kwa sasa matumizi ya mkaa yamekuwa makubwa kutokana na ongezeko la watu, ukataji wa miti umeongezeka na mpaka sasa kwa tafiti zilizopo zaidi ya tani milioni mbili za mkaa zimekuwa zikitumika kwa mwaka kama nishati ya kupikia majumbani, hali hiyo imeleta athari kubwa za kimazingira,” alisema Zungu.

Alisema mpango huo ambao utekelezaji wake bado  haujaanza, unalenga kuhudumia majiji makubwa na kwa Tanzania utaanza na  jijini la Dar es Salaam na kuenea katika majiji mengine kutokana na mafanikioyatakayopatikana.

“Pindi mazungumzo yatakapokamilika, awamu ya kwanza ya mradi huo utaanzia Dar es Salaam ambapo wakazi zaidi ya elfu kumi wanategemea kunufaika. Ni furaha kwetu iwapo mpango huu utakamilika kwani zaidi ya asilimia 90 ya wakazi wake wanatumia mkaa,” alisema

- Advertisement -
bestbettingafrica

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

66,457FansLike
167,522FollowersFollow
526,000SubscribersSubscribe
- Advertisement -
10Bet

Latest Articles