Waziri: Waajiri chanzo cha migogoro ya wafanyakazi

0
589
Naibu Waziri wa Utumishi wa umma Dk. Mary Mwanjelwa

Derick Milton, Simiyu

Naibu Waziri wa Utumishi wa umma Dk. Mary Mwanjelwa amesema waajiri wengi Nchini wamekuwa hawatimizi majukumu yao ipasavyo hali inayosababisha uwepo wa migogoro na changamoto nyingi katika sehemu zao za kazi.

Dkt. Mwanjelwa ameyasema hayo leo wakati akizungumza na baadhi ya watumishi wa umma  katika kikao kazi kilichofanyika kwenye ukumbi wa Shule ya Msingi Bariadi Allience Mjini Bariadi.

Amesema kuwa waajiri wengi wamekuwa wakijiona wao kuwa ni Mungu watu hivyo hata utendaji wao wa kazi umekuwa haufuati taratibu na kanuni za utumishi wa umma na kwamba mara nyingi wamekuwa wakifanya kazi  kwa mazoea na kusababisha uminyaji wa uhuru na haki za watumishi wa umma.

‘Sisi viongozi tuliopewa mamlaka husika ya kusimamia sekta ya utumishi wa umma ni lazima tusimamie sheria na taratibu zinazotakiwa hivyo basi serikali ya awamu ya tano kamwe haitaweza kulifumbia macho suala la waajiri hao kuwaonea na kuwanyanyasa waajiriwa wao,” amesema Dk Mwanjelwa.

Akitoa taarifa ya mkoa Katibu tawala wa mkoa, Jumanne Sagini amesema kuwa katika watumishi  12,053 wa Mkoa wa Simiyu, watumishi 2,285 walitakiwa wapandishwe vyeo kwa mwaka 2017-2018 lakini hadi sasa hawajapandishwa.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here