26.9 C
Dar es Salaam
Thursday, April 25, 2024

Contact us: [email protected]

Waziri wa Usalama wa Ndani wa Marekani ajiuzulu

WASHINGTON, MAREKANI

RAIS Donald Trump ametangaza kujiuzulu kwa Waziri wa Usalama wa Ndani, Kirstjen Nielsen, hatua inayosititiza nia yake ya kuimarisha sera ya uhamiaji.

Kuondoka kwa Nielsen kunahitimisha uhusiano mgumu na bosi wake, ambaye alisemekana kutofurahishwa na utendaji kazi wake licha ya utiifu mkubwa kwake na kuzitetea kikamilifu sera zake nyingi tata.

Wakati wa uongozi wake wa miezi 18 katika wizara hiyo yenye nguvu, Nielsen (46) alitambulika kwa utaratibu wenye utata wa kuwatenganisha watoto na wazaziwao.

Kwa sababu hiyo alilengwa mara kwa mara na makundi ya haki za binadamu na chama cha upinzani cha Democratic kilichokuwa kikimtaka ajiuzulu.

Hayo yote inaonekana hayakumridhisha Trump ambaye aliandika kwenye mtandao wa Twitter jana kuwa waziri huyo ataachia wadhifa huo, na akamshukuru kwa kazi yake.

Aliongeza kuwa Kamishna wa Forodha na Ulinzi wa Mipaka, Kevin McAleenan atakuwa kaimu waziri kuchukua nafasi ya Nielsen.

McAleenan ni ofisa wa muda mrefu wa ulinzi wa mipaka ambaye

anaheshimiwa na wabunge na ndani ya Serikali.

Kwenye barua yake ya kujiuzulu, Nielsen alisema licha ya hatua zilizopigwa katika kuufanyia mageuzi usalama wa ndani, umefikia wakati wa yeye kujiuzulu.

Hatua hiyo imekuja siku mbili tu baada ya yeye na Trump kuzuru kwa

pamoja eneo la mpaka wa Mexico, Jimbo la California, ambako rais alitoa ujumbe mkali kwa wanaopanga kuwa wahamiaji haramu na wanaoomba hifadhi akisema kuwa Marekani imejaa.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles