26.2 C
Dar es Salaam
Saturday, August 13, 2022

Waziri wa Mambo ya Nje Ujerumani azuru Afghanistan

KABUL, AFGHANISTAN

WAZIRI wa Mambo ya Nje wa Ujerumani, Heiko Maas ambaye yupo ziarani nchini hapa, amesema ziara yake inaonesha wazi jinsi Ujerumani ilivyojizatiti katika juhudi za kuleta suluhisho la amani katika mgogoro nchini hapa.

Maas aliwasili kwenye Jimbo la Mazar-e-Sharif kaskazini mwa nchi hii juzi kwa lengo la kutoa ujumbe wa kusisitiza msimamo wa Ujerumani juu ya kuendeleza juhudi za kuleta suluhisho la amani.

Ujerumani ni nchi mojawapo ya Jumuiya ya Kujihami ya NATO inayoiunga mkono Afghanistan kwa kutoa mafunzo kwa majeshi ya usalama na wanajeshi 1,200 wa taifa hilo wapo hapa kulinda amani.

Mwezi uliopita Bunge la Ujerumani liliongeza muda wa kuwepo wanajeshi hao nchini hapa na pia  Ujerumani inasema kwamba pia iko tayari kuandaa mkutano juu ya kuleta amani utakaowashirikisha pia wanamgambo wa Taliban.

Katika hotuba yake, Maas alisema lengo la kufanya ziara nchini hapa na Pakistan ni kutoa ujumbe wa wazi, kwamba Ujerumani imejizatiti katika kuutekeleza wajibu walioahidi kuutimiza juu ya nchi hii.

Ujerumani inashika nafasi ya pili kama mfadhili na pia imechangia majeshi nchini hapa.

Maas alisema kwamba Serikali ya Ujerumani inatekeleza sera ya kuihakikishia Afghanistan kwamba itaendelea kufanya juhudi za kuleta suluhisho la amani.

Pia kusaidia katika juhudi za kuleta maendeleo ya uchumi katika kanda inayopakana na Afghanistan.

Hata hivyo Maas amesisitiza kwamba kufanya mazungumzo na Taliban hakuna maana ya kurejea katika maafa ya miaka iliyopita.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
198,625FollowersFollow
550,000SubscribersSubscribe

Latest Articles